Old/New Testament
Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu
20 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu mwenye shamba la mizabibu aliyeondoka alfajiri kwenda kutafuta vibarua wa kufanya kazi shambani kwake. 2 Wakapatana kuwa atawalipa msha hara wa kutwa, yaani dinari moja, akawapeleka shambani.
3 “Mnamo saa tatu akaondoka tena akawakuta watu wengine wamesimama sokoni bila kazi. 4 Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu na nitawalipa haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda. 5 Mnamo saa sita na pia saa tisa alion doka tena akafanya hivyo hivyo. 6 Mnamo saa kumi na moja akaon doka tena akawakuta watu wengine bado wanazurura. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ 7 Wakamjibu, ‘Ni kwa kuwa hakuna aliyetuajiri.’ Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la miza bibu.’
8 “Ilipofika jioni, yule mwenye shamba akamwita msimamizi wa vibarua akamwambia, ‘Waite wafanyakazi uwalipe ujira wao, ukian zia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ 9 Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akalipwa dinari moja. 10 Basi wale wal ioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipewa dinari moja. 11 Walipoipokea, wakaanza kumlalamikia yule mwenye shamba wakisema, 12 ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu. Ime kuwaje wewe ukawalipa sawa na sisi ambao tumefanya kazi ngumu na kuchomwa na jua mchana kutwa?’
13 “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sija kudhulumu. Je, hatukupatana kwamba utafanya kazi kwa dinari moja? 14 Chukua haki yako uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu ali yeajiriwa mwisho sawa na wewe. 15 Je, siwezi kufanya nipendavyo na mali yangu? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’ 16 Hali kadhalika, wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”
Copyright © 1989 by Biblica