Old/New Testament
Hakuna Mwisho Wa Kusamehe
21 Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini.”
Mfano Wa Mdaiwa Asiyesamehe
23 “Kwa hiyo Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kukamilisha hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kukagua hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa na deni la mamilioni ya shilingi, aliletwa kwake. 25 Na kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake aliamuru kwamba auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vyote alivyo navyo, ili zipatikane fedha za kulipa deni lake.
26 “Yule mtumishi akapiga magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 27 Yule bwana akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwachilia.
28 “Lakini yule mtumishi alipotoka, alikutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha shilingi chache. Akamkamata, akam kaba koo akimwambia, ‘Nilipe deni langu!’
29 “Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 30 Lakini akaka taa. Badala yake akampeleka afungwe gerezani mpaka aweze kulipa hilo deni.
31 “Watumishi wenzake walipoona mambo haya, walisikitika sana. Wakamwendea bwana wao wakamweleza yote yaliyotokea.
32 “Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu, uliponisihi, nilikusamehe deni lako lote. 33 Je, hukupaswa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhuru mia?’ 34 Kwa hasira yule bwana akamkabidhi yule mtumishi kwa askari wa gereza mpaka atakapomaliza kulipa deni lote.
35 “Na hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ambaye hatamsamehe ndugu yake kwa moyo.”
Copyright © 1989 by Biblica