Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Exod for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matayo 15:21-39

21 Na Yesu akaondoka mahali hapo akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22 Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu hizo akaja kwake, akamlilia, akasema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa na pepo na anasumbuka sana.” 23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele. ” 24 Akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli wal iopotea.”

25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu akasema, “Bwana, nisaidie!” 26 Yesu akajibu, “Si haki kuchu kua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” 27 Yule mwanamke akajibu, “Ndio, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoan guka kutoka kwenye meza za mabwana wao.”

28 Ndipo Yesu akamwambia, “Mama, imani yako ni kubwa! Na ufanyiwe kama unavyotaka.” Tangu wakati huo mtoto wake akapona.

Yesu Aponya Watu Wengi

29 Yesu akaondoka mahali hapo akapita kando ya bahari ya Galilaya. Akapanda mlimani, akaketi huko . 30 Umati mkubwa wa watu wakamjia wakiwaleta viwete, vilema, vipofu, viziwi na wen gine wengi, wakawaweka karibu yake; naye akawaponya. 31 Watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Yesu Alisha Watu Elfu Nne

32 Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Nina waonea huruma watu hawa kwa maana wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. Sipendi kuwaaga wakiwa na njaa wasije wakazimia njiani.”

33 Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha watu hawa wote, nasi tuko nyikani?” 34 Na Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba, na samaki wadogo wachache.” 35 Yesu akaamuru watu wakae chini. 36 Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, akamshukuru Mungu, akavimega akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 37 Wote wakala, wakashiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 38 Idadi ya watu waliokula ilikuwa elfu nne bila kuhesabu wanawake na watoto.

39 Baada ya kuwaaga watu, Yesu akaingia katika mashua akaenda sehemu za Magadani.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica