Old/New Testament
Yesu Amponya Mtu Aliyepooza
9 Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. 2 Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” 3 Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” 4 Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa 6 Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” 7 Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. 8 Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.
Yesu Amwita Mathayo
9 Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Wakati Yesu alipo kuwa ameketi mezani kula chakula katika nyumba fulani, watoza kodi wengi na wenye dhambi walikuja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula na watoza kodi na wenye dhambi?” 12 Lakini Yesu alipowasikia aliwaambia, “ Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Napenda huruma na wala sio sadaka za kuteketeza.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga
14 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuja kwa Yesu wakamwuli za, “Mbona sisi na Mafarisayo tunafunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” 15 Yesu akawajibu, “Hivi inawezekana wageni wali oalikwa harusini kuomboleza wakati bwana harusi yuko nao? Wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo wataka pofunga. 16 Hakuna mtu anayeweka kiraka kipya kwenye nguo kuu kuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye nguo hiyo na tundu litakalotokea litakuwa kubwa zaidi ya lile la mwanzo. 17 Wala watu hawahifadhi divai mpya kwenye viriba vikuukuu; wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Lakini divai mpya huwekwa katika viriba vipya na kwa njia hiyo divai na viriba husalimika.”
Copyright © 1989 by Biblica