Old/New Testament
15 Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2 Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata mimi.” 4 Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini. 5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6 ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuhusu Umoja
7 Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea, ili Mungu apate kutukuzwa. 8 Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9 Na pia ili watu wa mataifa mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko: “Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba nyimbo za kulisifu jina lako.” 10 Na tena yanasema, “Ninyi watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.” 11 Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12 Na tena Isaya anasema:“Shina la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote; na watu wa ma taifa watamtumaini.”
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.
Copyright © 1989 by Biblica