Old/New Testament
Paulo Asafirishwa Kwenda Rumi
27 Ilipoamuliwa kwamba twende Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa askari mmoja aitwaye Juliasi ambaye alikuwa wa kikosi cha Kaisari Agusto. 2 Tulipakia meli iliyotoka Adrami tio ambayo ilikuwa ikielekea kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia. Tukaanza safari yetu tukiongozana na Aristarko, Mmakedonia wa kutoka Thesalonike. 3 Kesho yake tulifika Sidoni. Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kuwaona rafiki zake wam hudumie. 4 Kutoka huko tuliendelea na safari yetu, na kwa kuwa tulikuwa tunakabili upepo, tukapitia upande wa kisiwa cha Kipro usioelekea upepo. 5 Tukavuka bahari, kutoka upande wa Kilikia, na Pamfilia, tukafika Mira, katika jimbo la Likia. 6 Yule askari akapata meli iliyokuwa inatoka Aleksandria ikielekea Italia, akatupakia humo. 7 Tukasafiri pole pole kwa siku nyingi, na kwa shida na hatimaye tukafika karibu na bandari ya Nido. Lakini kwa kuwa upepo mkali ulikuwa ukivuma kutoka tulikokuwa tukielekea, hatukuweza kuendelea moja kwa moja na safari yetu, bali tulipitia upande wa pili wa Krete tukaizunguka ncha ya Salmone. 8 Baada ya kuizunguka kwa shida tulifika sehemu iitwayo Bandari Nzuri, kar ibu na mji wa Lasea.
9 Tulikuwa tumepoteza muda mrefu baharini na kwa wakati huu safari ilikuwa ya hatari kwa maana majira ya kufunga yalikuwa yamekwisha pita. Paulo akawaonya marubani wa ile meli akasema, 10 ‘ ‘Mabwana, naona tukiendelea na safari hii patatokea maafa na hasara kubwa kwa meli na shehena na hata maisha yetu yatakuwa hatarini.” 11 Lakini yule askari akaamua kusikiliza zaidi ushauri wa nahodha na mwenye meli kuliko maneno ya Paulo. 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba waendelee na safari na pengine kwa bahati wangeweza kufika Foinike. Hii ni bandari iliyoko katika kisiwa cha Krete na ambayo inatazama upande wa kusini-magharibi na kas kazini-magharibi, kwa hiyo wangeweza kukaa huko mpaka majira ya baridi yaishe.
Dhoruba Baharini
13 Upepo ulipoanza kuvuma taratibu toka kusini, wakadhani kuwa hii ilikuwa ni dalili nzuri kwamba wangeweza kuendelea na safari. Kwa hiyo wakang’oa nanga wakasafiri wakipita kando kando ya pwani ya kisiwa cha Krete. 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali uitwao ‘Kaskazi-mashariki’ ukavuma toka nchi kavu; 15 ukaipiga ile meli, na kwa kuwa haikuwa rahisi kushindana nao, tukaiachilia meli isukumwe kuelekea kule upepo unakokwenda. 16 Hatimaye tukasafiri kupitia nyuma ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. 17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee. 18 Kesho yake dhoruba kali iliendelea kuvuma, kwa hiyo wakaanza kuitupa shehena baharini. 19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. 20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.
21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii. 22 Lakini sasa nawaomba mjipe moyo. Hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake ila meli hii itaangamia. 23 Jana usiku, malaika wa Mungu wangu ambaye mimi namwabudu alisimama karibu yangu 24 akasema, ‘Usiogope Paulo; huna budi kujitetea katika kesi yako mbele ya Kaisari; na kwa neema yake, Mungu amekupa maisha ya watu wote wanaosafiri pamoja na wewe.’ 25 Kwa hiyo muwe na matu maini kwa maana nina imani kwa Mungu kwamba mambo yatakuwa kama nilivyoambiwa. 26 Lakini hata hiyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani. ”
Copyright © 1989 by Biblica