Old/New Testament
22 Lakini Sauli alizidi kuhubiri kwa nguvu zaidi akathibitisha kabisa kwamba Yesu ndiye Kristo; hata Wayahudi walioishi Dameski hawa kuwa na lo lote la kupinga. 23 Baada ya siku nyingi kupita, Way ahudi walifanya mpango wa kumwua Sauli. 24 Lakini Sauli akapata habari za mpango huo. Wayahudi walikuwa wakilinda milango yote ya kutokea mjini, mchana na usiku ili akitoka wamwue. 25 Lakini wanafunzi wake wakamtoa nje ya mji usiku kwa kumpitisha mahali palipokuwa na nafasi katika ukuta wa mji, akiwa ndani ya kapu kubwa.
Sauli Atoa Ushuhuda Wake Yerusalemu
26 Sauli alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na waamini lakini wao walimwogopa kwa maana hawakuamini ya kuwa kweli ali kuwa amemwamini Yesu. 27 Lakini Barnaba akamchukua Sauli akampeleka kwa wale mitume akawaeleza jinsi Sauli alivyokutana na Yesu njiani akienda Dameski na Yesu akasema naye. Pia akawaeleza jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Kwa hiyo Sauli akakaa nao akishirikiana nao na aki hubiri wazi wazi kwa jina la Yesu kila mahali huko Yerusalemu.
29 Lakini alipowahubiria Wayahudi wenye asili ya Kigiriki na kubishana nao, wao waliamua kumwua. 30 Waamini wengine walipo pata habari hizi walimchukua hadi Kaisaria wakamsafirisha kwenda Tarso. 31 Ndipo kanisa katika Yudea yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Kanisa likapata nguvu likienenda katika kicho cha Bwana; na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.
Petro Amponya Ainea
32 Petro alipokuwa akiwatembelea waamini sehemu mbalimbali alifika kwa watu wa Mungu walioishi huko Lida. 33 Akamkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya; inuka utandike kitanda chako.” Na mara Ainea akainuka. 35 Wakazi wote wa Lida na Sharoni wali pomwona Ainea akitembea walimgeukia Bwana.
Petro Amfufua Dorkasi
36 Huko Jopa kulikuwa na mwanafunzi mwanamke aliyeitwa Tabita au kwa lugha ya Kigiriki, Dorkasi, yaani paa. Huyu mama alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37 Hata hivyo aliugua akafa. Wakamwosha na kumlaza katika chumba cha ghorofani. 38 Kwa kuwa Jopa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kuwa Petro yuko Lida, waliwatuma wenzao wawili wakamwambie, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39 Kwa hiyo Petro akaharakisha akaenda nao Jopa. Alipowasili wakampeleka hadi kwenye chumba alipokuwa amelazwa marehemu Dor kasi. Wajane wengi walikuwa wamemzunguka marehemu wakilia na kuonyesha mavazi ambayo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa hai. 40 Petro akawatoa wote nje, kisha akapiga magoti akaomba; akaugeukia ule mwili akasema, “Tabita, Amka!” Dorkasi akafumbua macho na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamsaidia kusimama. Ndipo alipowaita wale waamini na wajane aka wakabidhi Dorkasi akiwa hai. 42 Habari hizi zilienea sehemu zote za Jopa. Na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Petro akakaa Jopa kwa muda mrefu, akiishi na mtengenezaji ngozi mmoja aitwaye
Copyright © 1989 by Biblica