Old/New Testament
22 “Nawasihi ninyi Waisraeli mnisikilize. Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa njia ya miujiza, maajabu na ishara, kama ninyi wenyewe mjuavyo. 23 Huyu Yesu ali tiwa mikononi mwenu kwa mpango na makusudi ya Mungu aliyoyafahamu tangu awali. Nanyi mlimwua kwa kumtundika na kumpigilia misumari msalabani, mkisaidiwa na watu waovu. 24 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu hata kifo kisingaliweza kumzuia. 25 Daudi alisema hivi juu yake, ‘Nilimwona Bwana akiwa mbele yangu wakati wote, Bwana yuko upande wangu wa kulia ili nisiogope. 26 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao una matumaini ya uzima. 27 Kwa maana wewe Bwana hutaniacha kuzimu; wala hutaacha mtakatifu wako ateseke na kuoza. 28 Wewe umenionyesha njia inifikishayo uzimani. Na uwepo wako ukiwepo nami nitajawa na furaha.’
29 “Ndugu zangu, nataka niwaambie wazi kwamba mfalme Daudi alikufa na kuzikwa, na kaburi lake lipo hata leo. 30 Lakini ali kuwa nabii, na alijua ya kuwa Mungu aliahidi kwa kiapo kwamba angempa mmoja wa uzao wake kiti chake cha ufalme. 31 Kwa hiyo Daudi akaona mambo ambayo yangetokea, akatamka juu ya kufufuka kwa Kristo, kwamba asingeachwa kuzimu, wala mwili wake usingehar ibiwa kwa kuoza. 32 Huyu Yesu, Mungu alimfufua, na sisi ni mash ahidi wa tukio hilo.
33 “Basi akiwa ametukuzwa na kukaa upande wa kulia wa Mungu, alipokea Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba yake. Huyo Roho Mtakatifu ndiye aliyetumiminia haya mnayoyaona na kuyasikia. 34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alim wambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’
36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye
Ongezeko La Waamini
37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?” 38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu anamwita kwake.”
40 Petro aliwasihi kwa maneno mengine mengi na kuwaonya akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kiovu.” 41 Wote waliopokea ujumbe wa Petro walibatizwa na zaidi ya watu elfu tatu wal iongezeka katika kundi la waamini siku hiyo.
Ushirika Wa Waamini
42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali. 43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu yalifanywa na mitume.
44 Waamini wote waliishi pamoja na kushirikiana kila kitu walichokuwa nacho kwa pamoja. 45 Waliuza mali zao na vitu waliv yokuwa navyo wakagawiana fedha walizopata, kila mtu akapata kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote waliendelea kuabudu katika Hekalu na kushiriki chakula cha Bwana nyumbani mwao na kula pamoja kwa furaha na shukrani, 47 huku wakimsifu Mungu na kupendwa na watu wote. Na kila siku Bwana alikuwa akiongeza katika kundi lao watu aliokuwa akiwaokoa.
Copyright © 1989 by Biblica