Old/New Testament
Kifo Cha Lazaro
11 Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika kijiji cha Bethania pamoja na dada zake wawili, Mariamu na Martha. 2 Huyu Mariamu ndiye aliyempaka Bwana Yesu manukato miguuni na kumpangusa kwa nywele zake. 3 Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” 4 Lakini Yesu alipopata habari hizi alisema, “Ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea ili kudhihirisha utu kufu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi Mwana wa Mungu, nitatukuzwa. ”
5 Kwa hiyo ijapokuwa Yesu aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro, 6 alipopata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukaa huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. 7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea.” 8 Wanafunzi wake wakam wambia, “Mwalimu, utakwendaje tena Yudea ambako siku chache tu zilizopita Wayahudi walitaka kukupiga mawe?” 9 Yesu akawajibu, “Si kuna masaa kumi na mawili ya mchana katika siku moja? Mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa maana kuna mwanga wa ulim wengu. 10 Lakini mtu akitembea usiku hujikwaa kwa sababu hana mwanga nafsini mwake.”
11 Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”
2 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.” 13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi. 14 Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa. 15 Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla Lazaro kufa. Hii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni.” 16 Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe pamoja naye.”
Yesu Ni Ufufuo Na Uzima
17 Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita. 18 Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu, 19 Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. 20 Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani. 21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa. 22 Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.” 23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.” 24 Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; 26 na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?” 27 Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.”
Yesu Analia
28 Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita.” 29 Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu.
Copyright © 1989 by Biblica