Old/New Testament
24 Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26 Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
34 Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35 Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38 lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”
39 Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.
40 Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 Na wengi wakamwamini Yesu.
Copyright © 1989 by Biblica