Old/New Testament
24 Kwa hiyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu wakamwambia, “Tuambie kweli mbele ya Mungu. Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.” 25 Akawajibu, “Kama yeye ni mwenye dhambi au sio, mimi sijui. Lakini nina hakika na jambo moja: nil ikuwa kipofu na sasa naona.”
26 Wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” 27 Akawajibu, “Nimekwisha waambia aliyonifanyia lakini hamtaki kusikia. Mbona mnataka niwaeleze tena? Au na ninyi mna taka kuwa wafuasi wake?” 28 Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ni mfuasi wake. Sisi ni wafuasi wa Musa. 29 Tunajua kwamba Mungu alisema na Musa. Lakini huyu mtu hatujui anakotoka.” 30 Akawa jibu, “Hii kweli ni ajabu! Hamjui anakotoka naye ameniponya upofu wangu! 31 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomwabudu na kumtii. 32 Haijawahi kutokea tangu ulimwengu kuumbwa kwamba mtu amemponya kipofu wa kuzaliwa. 33 Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufa nya lo lote.” 34 Wao wakamjibu, Wewe ulizaliwa katika dhambi! Utawezaje kutufundisha?” Wakamfukuzia nje.
Vipofu Wa Kiroho
35 Yesu alipopata habari kuwa yule mtu aliyemfumbua macho amefukuzwa kutoka katika sinagogi, alimtafuta akamwuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?” 36 Yule mtu akamjibu, “Tafadhali nifahamishe yeye ni nani ili nipate kumwamini.” 37 Yesu akam jibu “Umekwisha mwona naye ni mimi ninayezungumza nawe.” 38 Yule mtu akamjibu huku akipiga magoti, “Bwana, naamini.”
39 Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu; ili wale walio vipofu wapate kuona; na wale wanaodhani wanaona, waonekane kuwa vipofu.”
40 Baadhi ya Mafarisayo waliomsikia akisema hivi wakauliza, “Je, unataka kusema kuwa sisi pia ni vipofu?” 41 Yesu akawa jibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, hamngekuwa na hatia. Lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi bado mna hatia.”
Copyright © 1989 by Biblica