Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 6:22-44

Watu Wanamtafuta Yesu

22 Kesho yake, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo ya pili waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila waliondoka peke yao. 23 Lakini mashua nyingine kutoka Tiberia zilikuwa karibu zina fika mahali pale walipokula mikate baada ya Yesu kumshukuru Mungu. 24 Basi wale watu walipotambua kwamba Yesu hayupo hapo, wala wanafunzi wake hawapo, waliingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu kumtafuta.

Yesu Ni Mkate Wa Uzima

25 Walipomkuta Yesu ng’ambo ya ziwa wakamwuliza, “Rabi, umefika lini huku?” 26 Yesu akawajibu, “Ni wazi kwamba ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza ninayofanya, isipo kuwa mnanitafuta kwa sababu mlikula mikate mkashiba. 27 Msishug hulikie sana chakula kiharibikacho bali shughulikieni chakula kidumucho; chakula cha uzima wa milele. Chakula hicho, nitawapeni mimi Mwana wa Adamu, ambaye Baba Mungu mwenyewe amenithibit isha.”

28 Wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuonekane kuwa tunatenda kazi ya Mungu?” 29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.” 30 Wakamwambia, “Utafanya ishara gani ya muujiza, tuone ili tukuamini? Utafanya jambo gani? 31 Baba zetu walikula mana jangwani. Kama Maandiko yanavyosema, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni wakala.”’

32 Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni. Baba yangu ndiye anayewapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule aliyeshuka kutoka mbinguni na ambaye anatoa uzima kwa ulimwengu.”

34 Wakamwambia, “Bwana, tupatie mkate huo sasa na siku zote.

35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39 Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”

41 Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Huyu si Yesu mwana wa Yusufu? Na baba yake na mama yake si tunawajua? Anawezaje basi kutuambia kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”

43 Lakini Yesu akawaambia, “Acheni kunung’unika. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama Baba aliyenituma hakumvuta kwangu; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica