Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 5:25-47

25 Nina waambia hakika, wakati utafika, tena umekwisha timia, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wote watakaoisikia wata kuwa hai. 26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha Mwanae kuwa chanzo cha uzima. 27 Na amempa Mwanae mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.

28 “Msishangae kusikia haya. Wakati unakuja ambapo wafu wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini; wale waliot enda mema watafufuka na kuwa hai, na wale waliotenda maovu, wata fufuka na kuhukumiwa. 30 Mimi siwezi kufanya jambo lo lote kwa mamlaka yangu mwenyewe. Mimi nahukumu kufuatana na jinsi Mungu anavyoniambia. Na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufa nya nipendavyo, bali nafanya mapenzi yake yeye aliyenipeleka.”

Mashahidi Wa Yesu

31 “Kama ningekuwa najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingekuwa na uzito. 32 Lakini yupo mwingine anishuhudiaye na ninafahamu kwamba ushuhuda wake ni wa kweli. 33 Mliwapeleka wajumbe wenu kwa Yohana, naye akashuhudia iliyo kweli. 34 Si kwamba ninategemea ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 35 Yohana alikuwa taa iliy owaka na kuwaangazia, na kwa muda mlikubali kufurahia nuru yake.

36 “Lakini ninao ushuhuda mzito zaidi kuliko wa Yohana. Kazi ambayo Baba amenituma nikamilishe, naam , ishara hizi nina zofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye aliyenituma. 37 Na Baba aliyenituma naye amenishuhudia. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuiona sura yake. 38 Wala ujumbe wake hamuupokei maana hamumwamini aliyemtuma.

39 “Mnasoma Maandiko kwa bidii kwa maana mnafikiri kuwa humo mtapata uzima wa milele. Maandiko hayo hayo ndio yanayonish uhudia mimi. 40 Lakini mnakataa kuja kwangu kupata uzima.

41 “Mimi sitafuti kutukuzwa na watu. 42 Lakini, ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu na mnakataa kunipokea. Lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 44 Ndio maana hamwezi kuamini! Mnapenda sana kusifiana wenyewe kwa wenyewe wala ham jishughulishi kutafuta sifa kutoka kwake ambaye peke yake ndiye

Mungu!

45 “Msidhani kuwa mimi nitawashtaki kwa Baba. Anayewashtaki ni huyo Musa ambaye mnamwekea matumaini yenu. 46 Kama kweli mli kuwa mmemwamini Musa, mngaliniamini na mimi kwa maana aliandika kunihusu mimi. 47 Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Musa, mtaaminije ninayoyasema?”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica