Old/New Testament
Mwana Kondoo Wa Mungu
29 Kesho yake Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazameni! Huyu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwapo kabla sijazaliwa.’ 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja nikibatiza kwa maji kusudi apate kufahamika kwa watu wa Israeli.”
32 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akish uka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 Mimi nisingem tambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji ali kuwa ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 Mimi nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”
Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu
35 Kesho yake, Yohana alikuwapo pale pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesu akipita, alisema, “Tazameni! Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, walimfuata Yesu. 38 Yesu akageuka akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Rabi’ 39 Yesu akawajibu, “Njooni mkapaone!” Ilikuwa yapata saa kumi jioni. Basi wakaenda wakaona alipokuwa anaishi, wakashinda naye siku hiyo.
40 Mmojawapo wa hao wanafunzi wawili waliomfuata Yesu baada ya kusikia maneno ya Yohana, alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro. 41 Mara baada ya haya Andrea alikwenda kumtafuta ndugu yake akamwambia, “Tumemwona Masihi,” yaani Kristo. 42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa.” Tafsiri ya Kefa kwa Kigiriki ni Petro, maana yake ‘Mwamba’.
Yesu Anawaita Filipo Na Nathanaeli
43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akakutana na Filipo, akamwambia, “Nifuate.” 44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji ambapo Andrea na Petro walikuwa wanaishi. 45 Fil ipo naye akamtafuta Nathanaeli akamwambia, “Tumekutana na Yesu wa Nazareti mwana wa Yusufu, ambaye Musa katika Torati na pia Manabii waliandika habari zake.” 46 Nathanaeli akajibu, “Je, inawezekana kitu cho chote chema kikatoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo ukajionee mwenyewe.” 47 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akasema, “Huyu ni Mwisraeli halisi. Hana udanganyifu wo wote.” 48 Nathanaeli akamwuliza, “Umenifaha muje? ” Yesu akamjibu, “Nilikuona wakati ulipokuwa chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” 49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nimekuambia kwamba nili kuona chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo!” 51 Ndipo akawaambia, “Ninawaambia hakika, mtaona mbingu ikifunguka, na malaika wa Mungu wakienda mbinguni na kushuka juu yangu mimi Mwana wa Adamu.”
Copyright © 1989 by Biblica