Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Kgs for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 22:31-46

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

31 Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, shetani ameomba ruhusa kwa Mungu awapepete ninyi kama ngano. 32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipotee. Na utakaponirudia mimi, uwatie moyo ndugu zako.”

33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”

Kujiandaa Wakati Wa Hatari

35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga. 37 Kwa sababu, nawambieni, yale Maandiko yaliyosema kwamba ‘Alihesabiwa pamoja na wahalifu’ yananihusu mimi na hayana budi kutimizwa. Naam, yale yaliyoandikwa kunihusu mimi yanatimia.” 38 Wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna mapanga mawili.” Akawajibu, “Inatosha!. Yesu Asali Kwenye Mlima Wa Mizeituni

39 Ndipo Yesu akaondoka kuelekea kwenye mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, na wanafunzi wake wakamfuata. 40 Alipofika huko akawaambia wanafunzi, “Ombeni kwamba msiingie katika majaribu.” 41 Akaenda mbali kidogo nao, kama umbali anaoweza mtu kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike.” [ 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46 Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica