Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Sam for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 13:23-35

23 Mtu mmoja akamwuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” 24 Akajibu, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, wengi watataka kuingia na hawataweza. 25 Wakati mwenye nyumba ataka poamka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana utufungulie!’ Atawajibu, ‘Sijui mtokako!’ 26 Nanyi mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, ulifundisha katika mitaa yetu!’ 27 Lakini yeye atawajibu, ‘Sijui mtokako. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’ 28 Ndipo kutakuwapo na kilio na kusaga meno mtakapomwona Ibrahimu, Isaka na Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, wakati ninyi mkiwa mmetupwa nje. 29 Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi na kaskazini na kusini na wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa kar amuni katika Ufalme wa Mungu. 30 Hakika wapo watu ambao sasa wako mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wengine walio wa kwanza sasa watakaokuwa wa mwisho.” Yesu Aomboleza Juu Ya Yerusalemu

31 Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” 32 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha: ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa leo na kesho, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu. 33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.

34 “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, wewe uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwa kusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hukuniruhusu! 35 Sasa nyumba yako inaachwa tupu. Ninakuambia, hutaniona tena mpaka wakati ule uta kaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye katika jina la Bwana.”’

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica