Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Sam for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 11:1-28

11 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. Utupatie chakula chetu kila siku. Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10 Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11 “Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12 Au akimwomba yai atampa nge? 13 Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho

Yesu Na Beelzebuli

14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.

24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”

27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica