Old/New Testament
Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo
26 Basi wakawasili ng’ambo ya pili katika jimbo la Wagerasi. 27 Na aliposhuka katika mashua alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyepagawa na pepo. Kwa muda mrefu mtu huyu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. 28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kuu, “Unataka nini kwangu, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu?
Nakuomba, tafadhali usinitese!”
29 Wakati huo Yesu alikuwa ameanza kumwamuru yule pepo mchafu amtoke. Mara nyingi pepo huyo alimwingia na hata alipo fungwa na minyororo na kuwekwa chini ya ulinzi aliivunjilia mbali minyororo hiyo na kukimbilia jangwani akiwa ametawaliwa kabisa na pepo huyo. 30 Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jeshi’ 31 Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda shimoni kwenye kifungo cha mashetani.
32 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo karibu wakilisha kando kando ya mlima. Wale pepo wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe. Akawaruhusu.
33 Kwa hiyo wakamtoka yule mtu wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe likatimka mbio katika ule mteremko mkali wakatumbukia ziwani na kuzama. 34 Watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe waliona yaliyotokea, wakakimbia wakaeneza habari hizi mjini na mashambani.
35 Watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotokea. Wali pofika hapo alipokuwa Yesu wakamwona yule mtu aliyetokwa na pepo amekaa karibu na Yesu, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa sana. 36 Wale walioona mambo yalivyotokea wakawasimu lia wenzao jinsi yule mtu alivyoponywa. 37 Watu wote wa jimbo hilo la Wagerasi wakamwomba Yesu aondoke kwao, kwa sababu wali kuwa wamejawa na woga. Basi akaingia katika mtumbwi akaondoka.
38 Yule mtu aliyetolewa pepo akamsihi Yesu afuatane naye. Lakini Yesu akakataa, akamwambia: 39 “Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu aliyokufanyia Mungu.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza mji mzima mambo makuu Yesu aliyomfanyia.
Yesu Amfufua Binti Wa Yairo
40 Yesu aliporudi ng’ambo ya pili umati mkubwa wa watu ukam pokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea.
41 Wakati huo akaja mtu mmoja jina lake Yairo, kiongozi wa sinagogi. Akapiga magoti mbele ya Yesu akamwomba afike nyumbani kwake, 42 kwa kuwa binti yake mwenye umri wa miaka kumi na mbili, aliyekuwa mtoto wake wa pekee, alikuwa mgonjwa mahututi, karibu ya kufa. Yesu alipokuwa akienda, umati ulimsonga sana.
43 Katika umati huo alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, wala hakuna mganga aliyeweza kumponya. 44 Akaja nyuma ya Yesu, akam gusa pindo la vazi lake. Mara damu iliyokuwa ikimtoka ikakauka, akapona. 45 Yesu akauliza: “Nani amenigusa?” Kila mtu alipo kana Petro akasema, “Bwana, watu ni wengi mno wanaokusonga kila upande.” 46 Yesu akasema: “Kuna mtu aliyenigusa maana naona ya kuwa nguvu za kuponya zimenitoka.” 47 Yule mama alipofahamu ya kuwa amegundulika akaja huku akitetemeka akapiga magoti mbele ya Yesu. Akamweleza Yesu mbele ya watu wote kilichomfanya amguse, na jinsi alivyoponywa mara. 48 Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” 49 Wakati Yesu alipo kuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo kum wambia, “Binti yako amefariki. Hakuna sababu ya kuendelea kum sumbua Mwalimu.” 50 Lakini Yesu aliposikia haya alimwambia Yairo, “Usiogope. Uwe na imani na binti yako atapona.” 51 Wal ipofika kwa Yairo akawazuia watu wote wasiingie ndani isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, na baba na mama wa yule binti. 52 Watu waliokuwepo walikuwa wakilia na kuomboleza lakini Yesu akawaam bia, “Acheni kulia! Huyu binti hajafa ila amelala!” 53 Wao wakamcheka kwa dharau maana walijua amekwisha kufa. 54 Yesu akamshika yule binti mkono akamwita: “Binti, amka!” 55 Uhai ukamrudia, naye akasimama mara moja. Yesu akaamuru apewe chakula. 56 Wazazi wake wakastaajabu sana lakini Yesu akawakataza wasim wambie mtu alivyomfufua binti yao.
Copyright © 1989 by Biblica