Old/New Testament
Wapendeni Adui Zenu
27 “Sikieni niwaambie, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 28 Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza. 29 Mtu akikupiga kofi, mgeuzie na shavu la pili. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua na shati lako pia. 30 Aombae mpe, na mtu akichukua mali yako usidai urudishiwe. 31 Watendee wengine unavyopenda nao wakutendee. 32 Je, kuna sifa gani mnapowapenda watu wawapendao? Hata wasiomjua Mungu huwapenda wawapendao. 33 Tena kuna sifa gani mnapowatendea mema wale wanaowatendea mema? Hata wasiomjua Mungu hufanyiana hivyo. 34 Tena mnapowakopesha wale tu ambao mnategemea kuwa watawalipa, kuna sifa gani? Hata watu wasiomjua Mungu huwakopesha wenye dhambi wenzao wakiwa na hakika ya kurudishiwa mali yao yote. 35 Bali, wapendeni adui zenu, watendeeni mema. Wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo mtapata zawadi kubwa nanyi mtakuwa wana wa Mungu Aliye Juu. Yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na watu waovu. 36 Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.”
Msiwahukumu Wengine
37 “Msiwahukumu wengine nanyi hamtahukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa. 38 Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.”
Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.”
39 Pia akawapa mfano akasema, “Je, kipofu anaweza kumwon goza kipofu mwenzake? Si wote wawili watatumbukia shimoni? 40 Mwanafunzi hawezi kuwa mjuzi kuliko mwalimu wake, ila akihi timu, anaweza kuwa bingwa kama mwalimu wake. 41 Mbona unatazama sana kipande kilichoko katika jicho la mwenzako nawe huoni pande lililoko ndani ya jicho lako? 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, hebu, nikusaidie kutoa kipande hicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni pande hilo lililoko ndani ya jicho lako? Mnafiki wewe! Ondoa kwanza pande hilo ndani ya jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kuondoa kipande kili choko ndani ya jicho la ndugu yako.
43 “Hakuna mti bora uzaao matunda hafifu wala hakuna mti hafifu uzaao matunda bora. 44 Kila mti hutambuliwa kwa matunda yake. Tini hazichumwi kwenye michongoma wala zabibu hazichumwi kwenye majani mwitu. 45 Hali kadhalika mtu mwema hutambulikana kwa matendo yake mazuri yatokayo katika moyo mwema. Mtu mwovu pia hutenda maovu yatokanayo na uovu uliojaa ndani ya moyo wake. Mtu hunena yale yaliyojaa moyoni mwake.
46 “Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana’ nanyi hamfanyi ninay owaambia?
47 Nitawaambieni alivyo mtu anayesikia na kufanya ninay osema. 48 Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba akachimba chini na kujenga msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipotokea, yakaikumba ile nyumba wala haikutikisika, kwani ilikuwa na msingi imara. 49 Lakini yeye ayasikiaye maneno yangu na asiyafuate, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya mchanga bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ilianguka mara, na kuporomoka kabisa.”
Copyright © 1989 by Biblica