Old/New Testament
Bwana Wa Sabato
6 Siku moja ya sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya ngano, wakayafi kicha na kula punje zake. 2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnavunja sheria kwa kuvuna ngano siku ya sabato?”
3 Yesu akawajibu, “Ninyi hamsomi Maandiko? Hamjasoma alicho fanya Mfalme Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 4 Aliingia Hekaluni, akachukua ile mikate ya madhabahuni -ambayo huliwa na makuhani peke yao -akala, kisha akawapa na wafuasi wake wakala!” 5 Akaongezea kusema, “Mimi Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”
6 Ikawa siku nyingine ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi, na alikuwepo mtu ambaye mkono wake wa kuume uli kuwa umepooza. 7 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanangoja waone kama atamponya mtu siku ya sabato ili wapate sababu ya kumshtaki. 8 Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Kwa hiyo akamwam bia yule aliyepooza mkono, ’Njoo usimame hapa mbele ili kila mtu akuone.” Yule mtu akaja mbele. 9 Kisha Yesu akawageukia wale walimu wa sheria na Mafarisayo akasema, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya sabato - kutenda mema au kutenda mabaya? Kuokoa maisha au kuyaangamiza?” 10 Akawatazama watu wote waliokuwepo. Kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukapona kabisa! 11 Wale wakuu wakakasirika sana. Wakaanza kushauriana, “Tumfa nye nini huyu Yesu?’ ’
Kuchaguliwa Kwa Mitume Kumi Na Wawili
12 Siku moja Yesu alikwenda milimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 13 Asubuhi akawaita wanafunzi wake, na kati yao akachagua kumi na wawili akawapa cheo cha “mitume.” Majina yao ni haya: 14 Simoni, aliyemwita Petro; Andrea, nduguye Simoni; Yakobo; Yohana; Filipo; Bartholomayo; 15 Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Simoni, aliyeitwa Mzalendo; 16 Yuda, mwana wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ambaye baadaye alimsaliti Yesu.
Yesu Aponya Wengi
17 Akashuka pamoja nao akasimama mahali penye uwanja tambar are. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu waliotoka sehemu zote za Yudea na Yerusalemu na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walikuwa wamekuja kumsiki liza na kuponywa magonjwa yao. 18 Hata wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu nao walimjia akawaponya. 19 Na watu wote wali kuwa wanajitahidi kumgusa kwa maana walipofanya hivyo, nguvu zil ikuwa zikimtoka na kuwaponya wote.
20 Kisha akawatazama wanafunzi wake akasema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini kwa sababu Ufalme wa mbinguni ni wenu! 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa! Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka. 22 Mmebari kiwa ninyi watu watakapowachukia na kuwakataa na kuwatukana na kuharibu sifa yenu kwa ajili yangu. 23 Yatakapotokea haya fura hini na kuruka ruka kwa furaha kwa sababu zawadi kubwa imewekwa mbinguni kwa ajili yenu. Hata baba zao waliwatendea manabii wa zamani vivyo hivyo.
24 “Lakini ole wenu ninyi matajiri, kwa sababu mmekwisha pata furaha yenu! Ole wenu ninyi mlioshiba, maana mtaona njaa! 25 Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtalia na kuomboleza! 26 Ole wenu mtakaposifiwa na watu, kwani ndivyo baba zao walivy owasifu manabii wa uongo.”
Copyright © 1989 by Biblica