Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Josh for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 2:25-52

25 Na alikuwepo huko Yerusalemu mzee mmoja jina lake Simeoni ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Siku zote alikuwa akitarajia ukombozi wa Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Pia Roho Mtaka tifu alikuwa amemhakikishia kuwa hangekufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Kwa hiyo, akiwa ameongozwa na Roho Mtaka tifu, Simeoni alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto mikononi mwake akamshukuru Mungu akisema: 29 “Sasa Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako niende kwa amani kama ulivyoniahidi, 30 kwa sababu macho yangu yameuona wokovu 31 ulioandaa mbele ya watu wote, 32 nuru itakayowaangazia watu wa mataifa na kuleta utukufu kwa watu wako Israeli.” 33 Wazazi wa mtoto walistaajabu kwa yale yaliyokuwa yakisemwa kumhusu mtoto wao. 34 Simeoni akawabariki. Kisha akamwambia Mariamu, mama yake, “Mtoto huyu amechaguliwa na Mungu kwa makusudi ya kuanga mizwa na kuokolewa kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ya onyo kutoka kwa Mungu ambayo watu wengi wataikataa 35 ili kudhi hirisha mawazo yao ya ndani. Na uchungu kama kisu kikali utaku choma moyoni.” 36-37 ,Tena, alikuwepo Hekaluni nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti wa Fanueli, wa kabila la Asheri. Nabii Ana alikuwa mjane wa miaka themanini na minne naye alikuwa ameolewa kwa miaka saba tu mumewe akafariki. Yeye aliishi humo Hekaluni daima, akimwabudu Mungu na kuomba na kufunga.

38 Wakati huo huo, Ana alikuja mbele akamshukuru Mungu na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu. 39 Yusufu na Mariamu walipokamilisha mambo yote yaliyotakiwa na sheria ya Mungu, walirudi nyumbani kwao Nazareti katika Wilaya ya Galilaya. 40 Yesu aliendelea kukua, akawa kijana mwenye nguvu na hekima, akijaa baraka za

Mtoto Yesu Adhihirisha Hekima Yake

41 kila mwaka wazazi wake walikwenda Yerusalemu kushiriki katika siku kuu ya Pasaka. 42 Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama desturi ilivyokuwa. 43 Sikukuu ilipokwisha walianza safari ya kurudi nyumbani. Yesu akabaki Yerusalemu pasipo wazazi wake kujua. 44 Wao walidhani yupo nao kwenye msafara kwa hiyo wakaenda mwendo wa siku nzima. Walipotambua kwamba hawakuwa naye, walianza kumtafuta kati ya jamaa na marafiki. 45 Hawakumpata, kwa hiyo wakarudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu wakamkuta Hek aluni ameketi kati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwau liza maswali. 47 Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa na majibu aliyoyatoa.

48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Mama yake akamwul iza: “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Baba yako na mimi tume hangaika kukutafuta kila mahali kwa wasiwasi mkubwa.” 49 Lakini yeye akajibu: “Kwa nini mlihangaika kunitafuta? Hamkujua ninge kuwa hapa Hekaluni kwenye nyumba ya Baba yangu? 50 Lakini wao hawakuelewa maana ya jibu lake.

51 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii, na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote. 52 Basi Yesu akaendelea kuongezeka katika kimo na hekima, akipendwa na

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica