Old/New Testament
15 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” 3 Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?
Unasikia mashtaka yao!”
5 Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.
Yesu Ahukumiwa Kifo
6 Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . 7 Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. 8 Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. 9 Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.
12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”
15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.
Maaskari Wamdhihaki Yesu
16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
Yesu Asulubishwa
21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.
25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
Copyright © 1989 by Biblica