Old/New Testament
Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima Waovu
12 Yesu alianza kusema nao kwa kutumia mifano: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akalizungushia uzio, akachimba kisima cha kutengenezea divai na akajenga mnara. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima fulani kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba alimtuma mtumishi wake kwa hao wakulima kuchukua sehemu yake ya mavuno. 3 Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 4 Yule mwenye shamba akamtuma mtum ishi mwingine. Wale wakulima wakampiga kichwani, na kumfanyia mambo ya aibu. 5 Akapeleka mtumishi mwingine tena. Huyu, wakam wua. Akapeleka wengine zaidi, baadhi yao wakawapiga na wengine wakawaua. 6 Mwenye shamba akawa amebakiwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumtuma. Huyu alikuwa mwanae aliyempenda sana. Hatimaye akaamua kumtuma akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwanangu.’ 7 Lakini wale wakulima wakashauriana, ‘Huyu mwanae ndiye mrithi. Tumwue na urithi utakuwa wetu.’ 8 Wakamchukua, wakamwua, wakam tupa nje ya shamba. 9 Mnadhani yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja, awaue hao wakulima kisha alikodishe shamba lake kwa wak ulima wengine. 10 Hamjasoma Maandiko haya? ‘Lile jiwe waliloli kataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la msingi. 11 Jambo hili limefa nywa na Bwana, nalo ni la ajabu kwetu.’ ”
12 Viongozi wa Wayahudi wakatafuta njia ya kumkamata Yesu kwa sababu walifahamu kuwa mfano huo uliwasema wao. Lakini wali waogopa watu. Kwa hiyo walimwacha wakaondoka, wakaenda zao. Kuhusu Kulipa Kodi
13 Mafarisayo kadhaa na Maherode walitumwa kuja kumtega Yesu katika maneno yake. 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunafahamu kuwa wewe huwaambia watu ukweli pasipo kujali watu watasema nini. Wala hujali cheo cha mtu bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Je, ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kais ari? 15 Tulipe kodi hiyo au tusilipe?” Lakini Yesu alitambua hila yao. Akawaambia, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni sar afu niione.” 16 Wakamletea. Akawauliza, “Hii ni picha ya nani na hii ni sahihi ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”
17 Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kais ari na vya Mungu mpeni Mungu.” Jibu hili liliwastaajabisha sana.
Kuhusu Ufufuo wa Wafu
18 Kisha Masadukayo, ambao wanaamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, walimjia Yesu wakamwuliza swali wakisema, 19 “Mwalimu, Musa alituandikia agizo kuwa kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake hana budi kumwoa mjane huyo ili amzalie ndugu yake watoto. 20 Sasa walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa akafariki pasipo kupata mtoto. 21 Wapili akam woa yule mjane, naye akafariki bila kuacha mtoto. Ikawa hivyo hata kwa yule wa tatu. 22 Kwa kifupi, ndugu wote saba walimwoa huyo mjane lakini wote hawakuzaa naye. Hatimaye yule mama naye akafariki. 23 Sasa tuambie, wakati wa ufufuo, watakapofufuka wote, huyo mama aliyeolewa na ndugu wote saba, atakuwa mke wa nani?”
24 Yesu akawajibu, “Mmekosea kabisa kwa maana hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu.” 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni . 26 Na kuhusu ufufuo wa wafu: hamjasoma katika kitabu cha Musa, sehemu ile inayoelezea jinsi Mungu alivyozungumza na Musa kutoka katika kichaka akisema, ‘Mimi, ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? 27 Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”
Copyright © 1989 by Biblica