Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Num for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Marko 6:1-29

Watu Wa Nazareti Wamkataa Yesu

Yesu akaondoka mahali hapo, akaenda mji wa kwao, akifu atana na wanafunzi wake. Ilipofika siku ya sabato, alianza ku fundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia walishangaa. Wakasema, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya? Amepataje kuwa na hekima ya namna hii? Amepata wapi uwezo wa kutenda miujiza ya namna hii? Huyu si yule seremala mtoto wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake si tuko nao hapa?” Basi hawakumwamini.

Yesu akawaambia, ‘ ‘Nabii huheshimiwa kila mahali isipokuwa katika mji wake na kati ya jamaa na ndugu zake.” Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuwagusa wagonjwa wachache na kuwaponya. Alishangazwa sana na jinsi walivyokuwa hawana imani.

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili

Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.

Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mfuko, wala fedha. Ila wavae viatu lakini wasichukue nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo lenu kwao.”

12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache dhambi. 13 Wakawatoa watu wengi pepo, wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.

Kifo Cha Yohana Mbatizaji

14 Mfalme Herode akapata habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limefahamika kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” 15 Wengine walisema, “Huyo ni Eliya!” Na wengine wakasema, “Ni nabii kama wale manabii wa zamani.” 16 Lakini Herode ali posikia habari hizi alisema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji niliyem kata kichwa; amefufuka!” 17 Kwa maana Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, awekwe gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa kaka yake, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa. 18 Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali wewe kumwoa mke wa kaka yako.” 19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwe kea kinyongo Yohana akataka kumwua. Lakini hakupata nafasi, 20 kwa sababu Herode alimwogopa Yohana ambaye alifahamu kuwa ni mtu mwenye haki na mtakatifu, akawa anamlinda. Ingawa Herode alifadhaika sana kila alipomsikiliza Yohana, bado alipenda kumsi kiliza.

21 Baadaye Herodia alipata nafasi aliyokuwa akiitafuta. Wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa mfalme Herode, mfalme alifanya sherehe kubwa, akawaalika viongozi wakuu wa ikulu, makamanda wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. 22 Binti yake Herodia akaja akacheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake. Mfalme Her ode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” 23 Akala kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu, nitakupa.”

24 Yule binti akaenda akamwuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akajibu, “Mwombe kichwa cha Yohana Mbati zaji.” 25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia .” 26 Mfalme akajuta sana, lakini hakuweza kumkatalia kwa kuwa alikuwa ameapa mbele ya wageni wake, na hakupenda kuvunja ahadi yake. 27 Kwa hiyo Herode akamtuma mmojawapo wa walinzi wake mara moja akamwagiza alete kichwa cha Yohana. 28 Yule mlinzi akaenda gerezani akamkata Yohana kichwa kisha akakileta kwenye sinia akampa yule binti; naye akampatia mama yake.

29 Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, walikuja wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica