Old/New Testament
Kondoo Na Mbuzi
31 “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake pamoja na malaika wote, ataketi katika kiti chake cha utukufu cha enzi. 32 Watu wa mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawaten ganisha kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi. 33 Atawaweka kondoo upande wa kulia na mbuzi upande wa kushoto. 34 Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wa kulia, ‘Njooni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mlioandaliwa tangu mwanzo wa dunia. 35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; 36 nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’
37 “Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? 38 Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha? 39 Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
40 “Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.’
41 “Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake. 42 Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu na hamkunipa kitu cha kunywa; 43 nilikuwa mgeni wala hamkunikaribisha; nilikuwa uchi hamkuni vika; na nilikuwa mgonjwa na gerezani nanyi hamkuja kunitazama.’
44 “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au ukihitaji nguo, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’
45 “Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kwa jinsi ambavyo hamkumfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkuni fanyia mimi.’
46 “Basi hawa wataingia katika adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”
Copyright © 1989 by Biblica