Old/New Testament
Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo
23 Kisha Yesu akawaambia ule umati wa watu pamoja na wana funzi wake: 2 “Walimu wa sheria na Mafarisayo wamechukua nafasi ya Musa, 3 kwa hiyo watiini na kufanya yote wanayowaambia mfa nye. Lakini msifuate matendo yao; kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuwabebesha watu, lakini wao wenyewe hawajaribu hata kunyoosha kidole kuisogeza!
5 “Wao hufanya mambo yao yote ili waonekane na watu. Wanavaa vipande vipana vya ngozi vilivyoandikwa sheria na kurefusha zaidi pindo za mavazi yao ya sala. 6 Wanapenda kukaa viti vya wageni wa heshima karamuni na viti vya mbele katika masinagogi. 7 Hupenda kuamkiwa masokoni na kuitwa ‘Rabi.’
8 “Lakini ninyi msipende kuitwa ‘Rabi’ kwa sababu mnaye rabi mmoja, na ninyi nyote ni ndugu. 9 Na msimwite mtu ye yote hapa duniani ‘baba’ kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni. 10 Hali kadhalika msipende kuitwa ‘mabwana’ kwa maana mnaye Bwana mmoja tu, yaani Kristo. 11 Aliye mkuu kuliko ninyi nyote atakuwa mtumishi wenu. 12 Ye yote anayejikuza atashushwa; na ye yote anayejinyenyekeza atainuliwa.
13 “Lakini ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnafungia watu milango ya Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, wala hamruhusu wale ambao wange penda kuingia waingie. [
14 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnadhulumu nyumba za wajane, na kwa kujionyesha kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.”]
15 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja awe mfuasi wa dini yenu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya astahili kwenda Jehena mara mbili zaidi yenu!
16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mnasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu iliyoko Hekaluni, itambidi atimize kiapo hicho.’ 17 Ninyi vipofu wajinga! Ni kipi kilicho bora zaidi, ni ile dhahabu au ni Hekalu ambalo ndilo linafanya dhahabu hiyo kuwa takatifu? 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyoko madhabahuni itambidi atimize kiapo hicho.’ 19 Ninyi vipofu! Ni kipi bora zaidi, sadaka, au madhabahu ambayo ndio inafanya sadaka hiyo kuwa takatifu? 20 Kwa hiyo mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hiyo madhabahu na vitu vyote vilivyoko juu yake. 21 Na mtu anapoapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na huyo aishie ndani yake. 22 Naye anayeapa kwa mbingu anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.
Copyright © 1989 by Biblica