Old/New Testament
Mfano Wa Karamu Ya Harusi
22 Yesu akazungumza nao tena kwa kutumia mifano, akasema, 2 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja ali yemwandalia mwanae karamu ya harusi. 3 Akawatuma watumishi wake wakawaite wageni walioalikwa lakini wakakataa kuja. 4 Akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni waalikwa kwamba karamu iko tayari, nimekwisha chinja fahali wangu na ng’ombe wanono kwa ajili yenu, karibuni karamuni.’ 5 Lakini waalikwa wakadharau, mmoja akaenda shambani kwake, mwingine akaenda kwenye miradi yake, 6 na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatendea mambo ya aibu na kuwaua.
7 “Yule mfalme akakasirika, akapeleka jeshi lake likawaanga miza wale wauaji na kuteketeza mji wao. 8 Kisha akawaambia watum ishi wake, ‘Karamu ya harusi ni tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja karamuni. 9 Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkawaalike harusini wote mtakaowakuta.’ 10 Wale watumishi wakaenda mabarabarani wakawakusanya wote waliowakuta, wema na wabaya. Ukumbi wa sherehe ya harusi ukajaa wageni.
11 “Lakini mfalme alipoingia kutazama wageni, alimwona mle ndani mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la harusi. 12 Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje humu bila vazi la harusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. 13 Basi mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ 14 Kwa maana walioitwa ni wengi lakini walioteuliwa ni wachache.”
Kuhusu Kulipa Kodi
15 Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17 Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”
18 Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20 Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?” 21 Wakamjibu, “Ni za Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”
22 Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.
Copyright © 1989 by Biblica