Old/New Testament
Mafundisho Ya Mafarisayo
15 Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo kutoka Yerusalemu walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 2 “Mbona wanafunzi wako hawafu ati mafundisho ya wazee wetu? Kwa maana wao hawanawi mikono ka bla ya kula!” 3 Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnazivunja amri za Mungu kwa ajili ya mafundisho yenu? 4 Kwa maana Mungu alisema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 5 Lakini ninyi mnasema kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kuku saidia nacho nimekitoa kwa Mungu,’ basi hana wajibu tena wa kum saidia baba yake. 6 Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 7 Ninyi wanafiki! Isaya alisema sawa juu yenu alipotabiri kwamba: 8 ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. 9 Kuniabudu kwao ni bure, na mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu.’ ”
Usafi Wa Kweli
10 Yesu akaita ule umati wa watu akawaambia, “Sikilizeni kwa makini na mwelewe: 11 kinachomfanya mtu kuwa mchafu mbele ya Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” 12 Kisha wanafunzi wake wakaja wakamwambia, “Unafahamu kwamba Mafarisayo walichukizwa sana na yale maneno uliyosema?”
13 Akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hakuupanda, utang’olewa. 14 Waacheni; wao ni viongozi vipofu. Na kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”
15 Petro akasema, “Tuambie maana ya mfano huo.” 16 Yesu akawauliza, “Hata na ninyi bado hamwelewi? 17 Hamtambui kwamba cho chote kiingiacho mdomoni hupitia tumboni na hatimaye hutolewa nje? 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kinachomfanya mtu kuwa mchafu. 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo machafu, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na matukano. 20 Haya ndio yamchafuayo mtu, lakini kula bila kunawa mikono hakumchafui mtu.”
Copyright © 1989 by Biblica