Old/New Testament
Yesu Atembea Juu Ya Maji
22 Baadaye Yesu akawaambia wanafunzi wake watangulie kwe nye mashua waende ng’ambo ya pili ya ziwa, wakati yeye anawaaga wale watu. 23 Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa hapo peke yake. 24 Wakati huo ile mashua ilikwisha fika mbali, ikisukwa sukwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa mkali.
25 Ilipokaribia alfajiri, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26 Lakini wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu. Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu. 27 Lakini mara moja Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi; msiogope.”
28 Petro akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29 Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka katika mashua, akatembea juu ya maji akimfuata Yesu. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”
31 Mara Yesu akanyoosha mkono wake, akamshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini ulikuwa na shaka?” 32 Na walipoingia katika mashua, upepo ukakoma. 33 Wote waliokuwamo katika mashua wakamwabudu wakisema, “Hakika, wewe ni Mwana wa
Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti
34 Walipokwisha kuvuka, wakafika Genesareti. 35 Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani na watu wakawaleta wagonjwa wote kwake 36 wakamsihi awaru husu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.
Copyright © 1989 by Biblica