Old/New Testament
Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa
14 Wakati huo, mfalme Herode alisikia habari za Yesu; 2 akawaam bia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu; ndio sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”
3 Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gere zani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake. 4 Kisa che nyewe ni kwamba Yohana alikuwa amemwambia Herode kuwa, “Si halali kwako kumwoa huyo mwanamke.” 5 Herode alitaka sana kumwua Yohana lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. 6 Lakini siku ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu walioalikwa akamfurahisha sana Herode. 7 Naye akaahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. 8 Kwa kushawishiwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9 Mfalme akajuta; lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, aliamuru kwamba ombi lake litekelezwe. 10 Akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani, 11 na kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.
12 Wanafunzi wa Yohana wakaja, wakauchukua mwili wake wakau zika. Kisha wakaenda, wakamwambia Yesu.
Yesu Alisha Zaidi Ya Watu Elfu Tano
13 Yesu aliposikia haya, aliondoka kwa mashua akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu wal ipata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu, kutoka mij ini. 14 Yesu alipofika kando ya bahari aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.
15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walimfuata wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na siku imekwisha. Waage watu waondoke ili wakajinunulie chakula vijijini.” 16 Yesu akasema, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Leteni hapa.” 19 Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20 Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.
Copyright © 1989 by Biblica