Old/New Testament
21 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanae auawe. Watoto nao wataasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka. 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwa maana nawaambieni hakika, hamtamaliza kuipitia miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajafika.
24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25 Inatosha ikiwa mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamethubutu kum wita bwana mwenye nyumba Beelzebuli, je, si watawasema vibaya zaidi jamaa ya mwenye nyumba?”
Anayestahili Kuogopwa
27 Ninalo waambia gizani, ninyi litamkeni mwangani: na lile mnalosikia likinong’onwa, litangazeni mkiwa mmesimama kwenye paa la nyumba. 28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehena. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 32 Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Lakini ye yote atakayenikana mbele ya watu, mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”
Gharama Ya Kumfuata Yesu
34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita. 35 Kwa maana nimekuja kuleta kutokuele wana kati ya mtu na baba yake, na kati ya binti na mama yake, na kati ya mkwe na mama mkwe wake. 36 Na maadui wakubwa wa mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake. 37 Ye yote anayempenda baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Na ye yote ampendaye mwanae au binti yake kuliko anavyoni penda mimi, hastahili kuwa wangu. 38 Na ye yote asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 39 Ata kayeng’ang’ania nafsi yake ataipoteza lakini aipotezae nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.”
Watakaopokea Tuzo
40 “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye ali yenituma. 41 Mtu anayemkaribisha nabii kwa kuwa ni nabii, atapo kea tuzo ya nabii; na mtu anayemkaribisha mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea tuzo ya mwenye haki. 42 Na mtu ata kayetoa japo kikombe cha maji kwa mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, basi ninawaambieni hakika, hatakosa tuzo yake.”
Copyright © 1989 by Biblica