Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matayo 10:1-20

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili

10 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. 10 Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.

11 “Mkiingia katika mji au kijiji cho chote, mtafuteni mtu mwaminifu mkae kwake mpaka mtakapoondoka. 12 Kila nyumba mtakay oingia, toeni salamu. 13 Kama watu wa nyumba hiyo wanastahili, amani yenu na ikae kwao; na kama hawastahili, amani yenu itawaru dia ninyi. 14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”

Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica