Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matayo 9:18-38

Yesu Amponya Mwanamke Aliyetokwa Damu

18 Wakati Yesu akiwa anawaambia haya, akaja afisa fulani akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amefariki lakini tafadhali uje umwekee mkono wako juu yake naye atakuwa hai.” 19 Yesu akasimama akamfuata. Wanafunzi wake pia wakaan damana naye.

20 Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona.

Yesu Amfufua Binti Wa Afisa

23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule afisa, aliwakuta waom bolezaji wanapiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele. 24 Akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25 Lakini watu walipok wisha tolewa nje, aliingia ndani akamshika mkono yule binti, naye akaamka. 26 Habari hizi zikaenea wilaya ile yote.

Yesu Aponya Vipofu

27 Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 28 Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?” Wakamjibu, “Ndio Bwana.” 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.” 30 Macho yao yakafunguka. Naye akawaonya, “Angalieni mtu ye yote asijue jambo hili.” 31 Lakini wao walipoondoka walieneza sifa zake katika ile wilaya yote.

Yesu Amponya Bubu

32 Walipokuwa wakiondoka, watu walimletea mtu bubu, ali yekuwa amepagawa na pepo. 33 Na yule pepo alipofukuzwa, yule aliyekuwa bubu aliweza kusema. Ule umati wa watu wakastaajabu, wakasema, “Jambo kama hili halijawahi kuonekana katika Israeli.” 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”

Wafanyakazi Ni Wachache

35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.

37 Akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini wafa nyakazi ni wachache; 38 basi mwombeni Bwana wa mavuno ili awape leke wafanyakazi kwenye mavuno yake.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica