Old/New Testament
18 Yesu alipoona umati wa watu unazidi kuongezeka aliwaamuru wanafunzi wake wavuke, waende ng’ambo ya pili. 19 Na mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu akamwambia, “Mwalimu, mimi nitaku fuata po pote utakapokwenda.” 20 Lakini Yesu akamjibu, “Mbweha wana mashimo yao, na ndege wa angani wana viota vyao, lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulaza kichwa changu.” 21 Mwana funzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” 22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, waache wal iokufa wawazike wafu wao.”
Yesu Atuliza Dhoruba
23 Alipoingia kwenye mashua wanafunzi wake walimfuata. 24 Mara dhoruba kali ikavuma na mawimbi yakakaribia kuzamisha ile mashua; lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakaenda kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunaangamia!”
26 Lakini Yesu akawajibu, “Enyi wenye imani haba, mbona mnaogopa?” Akasimama, akaikemea dhoruba na mawimbi; navyo vikat ulia, pakawa shwari kabisa. 27 Wanafunzi wake wakashangaa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu, ambaye hata upepo na bahari vinamtii?”
28 Walipofika ng’ambo ya Genezareti, watuwawili wenye pepo walikutana naye. Watu hawa waliishi makaburini na walikuwa wanat isha, kiasi kwamba hakuna mtu aliyethubutu kupita njia ile. 29 Wakapiga kelele, “Unataka nini kwetu, wewe Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kutimia?” 30 Mbali kidogo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Ukitufukuza, tafadhali turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.” 32 Akawaambia, “Nendeni”. Basi waka toka wakawaingia wale nguruwe; na kundi lote likatimka mbio kuelekea ukingoni mwa bahari, wakaangamia katika maji. 33 Wachungaji wa hao nguruwe wakakimbilia mjini wakaeleza kila kitu, na yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo. 34 Watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Wali pomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Copyright © 1989 by Biblica