Old/New Testament
Imani
11 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona. 2 Maana ni kwa imani wazee wa kale walipata kibali cha Mungu.
3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vinavyoonekana vilitengenezwa kutokana na vitu visiv yoonekana.
4 Kwa imani Abeli alimtolea Mungu sadaka bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alikubaliwa kuwa mtu mwenye haki, Mungu aliposi fia sadaka zake. Na kwa imani yake bado anasema ingawa amekufa.
5 Kwa imani, Enoki alichukuliwa mbinguni ili asife, hakuone kana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Basi, kabla haja chukuliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu. 6 Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.
7 Kwa imani Noe alipoonywa na Mungu kuhusu mambo yaliyokuwa hayajaonekana bado, alitii akajenga safina kuokoa jamii yake. Kwa sababu hii aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatika nayo kwa imani.
8 Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende kwenye nchi ambayo Mungu angempa kama urithi. Naye aliondoka akaenda ingawa hakujua aendako. 9 Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi ya ahadi. Aliishi katika nchi ya ugenini katika mahema pamoja na Isaki na Yakobo ambao pia walikuwa warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akitazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao umebuniwa na kujengwa na Mungu mwenyewe.
11 Kwa imani Sara alipewa uwezo wa kupata mimba ijapokuwa alishapita umri wa kuzaa, kwa sababu aliamini kwamba Mungu ali yemwahidi ni mwaminifu na angelitimiza ahadi yake. 12 Kwa hiyo kutokana na huyu mtu mmoja, ambaye alikuwa sawa na mfu, walizal iwa wazao wengi kama nyota za mbinguni na kama mchanga usiohesa bika wa pwani.
13 Watu wote hawa walikuwa bado wanaishi kwa imani walipo kufa. Hawakupata yale waliyoahidiwa; lakini waliyaona na kuyafu rahia kwa mbali. Nao walikiri kwamba walikuwa ni wageni wasiokuwa na maskani hapa duniani. 14 Maana watu wanaosema maneno kama hayo, wanaonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Kama walikuwa wakifikiria kuhusu nchi waliyoiacha, wangali pata nafasi ya kurudi huko. 16 Lakini sasa wanatamani nchi iliyo bora zaidi, yaani, nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa maana amewatayarishia mji.
17 Kwa imani Abrahamu alipojaribiwa alimtoa Isaki awe dha bihu. Yeye ambaye alikuwa amepokea ahadi za Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanae wa pekee awe dhabihu, 18 ingawa Mungu alikuwa amemwambia, “Uzao wako utatokana na Isaki.” 19 Abrahamu aliamini kwamba Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu, na kweli ni kama alimpata tena Isaka kutoka katika kifo.
Copyright © 1989 by Biblica