Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Isa for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Waefeso 5:17-33

17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali muelewe yaliyo mapenzi ya Mungu. 18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica