Previous Prev Day Next DayNext

New Testament in a Year

Read the New Testament from start to finish, from Matthew to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Matayo 21:23-46

Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

23 Yesu alipoingia tena Hekaluni, makuhani wakuu na wazee walimjia alipokuwa akifundisha, wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani na ni nani amekupa mamlaka hayo?” 24 Yesu akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali na mkinijibu nami nita waambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Mbinguni au kwa watu?” Wakaanza kubishana kati yao wakisema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema ulitoka kwa wanadamu, tunaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.” 27 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatufahamu.” Naye aka waambia, “Nami sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wana Wawili

28 ‘Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili wa kiume. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ 29 Yule mwanae akasema, ‘Siendi,’ lakini baadaye akabadili mawazo akaenda. 30 Kisha yule baba akamwendea yule mwanae mwingine akamwambia vile vile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda baba,’ lakini asiende. 31 Ni yupi kati yao aliyetimiza alivyotaka baba yake?” Wakamjibu, “Yule wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu.

32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kum wamini.”

Mfano Wa Wapangaji Waovu

33 “Sikilizeni mfano mwingine: mtu mmoja mwenye shamba alilima shamba akapanda mizabibu. Akalizungushia ua, na ndani yake akachimba kisima cha kusindikia zabibu; na akajenga mnara. Kisha akalikodisha hilo shamba kwa wakulima fulani, akasafiri kwenda nchi nyingine.

34 “Wakati wa mavuno ulipokaribia aliwatuma watumishi wake kwa hao wakulima kupokea mavuno yake. 35 Wale wakulima wakawaka mata wale watumishi; wakampiga mmoja, wakamwua mwingine na kum piga mawe mwingine. 36 Akatuma watumishi wengine, wengi kuliko wale wa mwanzo. Wale wakulima wakawatendea vile vile. 37 Mwish owe akamtuma mwanae kwao akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwa nangu.’ 38 Lakini walipomwona mwanae, waliambiana, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumwue tuchukue urithi wake.’ 39 Basi wakamchu kua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. 40 Sasa, akija yule mwenye shamba, mnadhani atawafanya nini hao waku lima?” 41 Wakamjibu, “Atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake kwa wakulima wengine ambao watampatia matunda yake wakati wa mavuno.”

42 Yesu akawaambia, “Hamjapata kusoma katika Maandiko kwamba: ‘Lile jiwe walilokataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la pembeni; Bwana ndiye amefanya jambo hili nalo ni zuri ajabu machoni petu’?

43 Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na watapewa watu wawezao kutoa matunda yake.” [ 44 “Na ambaye ataanguka kwenye jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagika sagika.”]

45 Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia mifano yake, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 46 Wakatafuta njia ya kumkamata lakini waliogopa ule umati wa watu kwa kuwa wao walim tambua Yesu kuwa nabii.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica