M’Cheyne Bible Reading Plan
Wimbo Wa Ushindi
19 Baada ya haya nikasikia sauti kama sauti kuu ya umati mkubwa wa watu mbinguni ikisema kwa nguvu, “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni wa Mungu wetu. 2 Maana hukumu zake ni za kweli na haki, amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uasherati wake. Mungu amelipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.” 3 Kwa mara nyingine wakasema kwa nguvu, “Hale luya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” 4 Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai walianguka kifudifudi wakamwabudu Mungu aliyekuwa ameketi katika kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu, “Amina! Hale luya!”
5 Na sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Msi funi Mungu wetu ninyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”
6 Kisha nikasikia sauti kama sauti ya umati mkubwa wa watu, kama sauti ya maporomoko ya maji mengi na kama ngurumo kuu ya radi kubwa ikisema, “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwe nyezi anatawala. 7 Tufurahi na kushangilia na kumtukuza maana harusi ya Mwana-Kondoo imefika na bibi harusi wake amejitayar isha. 8 Alipewa kitani safi nyeupe inayong’aa ili avae.” Hiyo kitani safi ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Na malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wal ioalikwa kwenye karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo.”’ Na akaniambia, “Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”
10 Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako wanaoshikilia ushuhuda wao kwa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio kiini cha unabii.”
Aliyepanda Farasi Mweupe
11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na mbele yangu nikaona farasi mweupe! Aliyeketi juu ya huyo farasi aliitwa Mwaminifu na Kweli, naye huhukumu na kupigana vita kwa ajili ya haki. 12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna vilemba vingi; na ameandikwa jina ambalo hakuna mwingine anayeli jua isipokuwa yeye mwenyewe. 13 Amevaa vazi lililochovywa katika damu na jina analoitwa ni “Neno la Mungu”. 14 Na majeshi ya mbinguni yaliyovaa kitani safi nyeupe walimfuata wakiwa wamepanda farasi weupe.
15 Kinywani mwake mlitoka upanga mkali wa kuyapiga mataifa. Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kukamua divai katika mtambo wa kutengenezea divai ya ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16 Kwenye vazi lake na paja lake liliandikwa jina hili: “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”
Bwana wa mabwana.”
17 Kisha nikamwona malaika amesimama ndani ya jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu. 18 Njooni mle nyama ya wafalme na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari; nyama ya farasi na wapanda farasi, nyama ya wanadamu wote, wakubwa kwa wadogo, watumwa na watu huru.”
19 Na nikamwona yule mnyama na wafalme wa duniani pamoja na majeshi yao wakikusanyika kumpiga vita yeye aketiye juu ya yule farasi pamoja na jeshi lake. 20 Yule mnyama akatekwa pamoja na yule nabii wa uongo, aliyefanya ishara za uongo, kwa niaba yake, akawadanganya wale waliopokea alama ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. 21 Waliobakia waliuawa kwa upanga wa yule aketiye juu ya farasi, kwa ule upanga utokao kinywani mwake; na ndege wote wakala nyama yao mpaka wakakinai.
Yesu Akamatwa
18 Baada ya sala hii Yesu aliondoka na wanafunzi wake waka vuka kijito cha Kidroni wakaingia katika bustani iliyokuwa upande wa pili. 2 Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. 3 Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. 4 Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5 Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia, “Ni mimi.” Yuda ambaye alimsaliti alikuwa amesimama na wale askari. 6 Yesu alipowaambia, ‘Ni mimi,’ walirudi nyuma wakaanguka chini! 7 Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakajibu, “Yesu wa Nazareti .” 8 Yesu akawaambia, “Nimekwisha waeleza kuwa ni mimi; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi waachilieni hawa wengine waende.” 9 Alisema haya ili lile neno alilosema lipate kutimia, ‘Kati ya wale ulionipa sikupoteza hata mmoja.’ 10 Ndipo Simoni Petro akachomoa upanga aliokuwa amechukua akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo lilikuwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?” 12 Kwa hiyo mkuu wa kikosi na askari wake pamoja na wale walinzi wa Hekalu waliot umwa na viongozi wa Wayahudi, wakamkamata Yesu wakamfunga mikono. 13 Kisha wakampeleka kwanza kwa Anasi mkwewe Kayafa ambaye ali kuwa ndiye kuhani mkuu mwaka ule. 14 Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri viongozi wengine wa Kiyahudi kwamba ingekuwa afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Petro Anamkana Yesu
15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu kwa hiyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 16 Lakini Petro alisimama nje karibu na mlango. Ndipo yule mwanafunzi mwin gine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda mlangoni, akamru husu amwingize Petro ndani. 17 Yule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro aka jibu, “Hata! Mimi sio.” 18 Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa mkaa ambao walikuwa wamewasha kwa sababu pale ukumbini palikuwa na baridi kali. Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
Kuhani Mkuu Amhoji Yesu
19 Kuhani mkuu akamwuliza Yesu maswali kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza wazi wazi mbele ya watu wote. Nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sijasema jambo lo lote kwa siri. 21 Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize walionisiki liza nimewaambia nini. Wao wanajua niliyosema.” 22 Mmoja wa wale walinzi akampiga Yesu kofi, kisha akasema, “Unathubutuje kumjibu kuhani mkuu hivyo?” 23 Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo baya waeleze watu wote hapa ubaya niliosema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” 24 Ndipo Anasi akampeleka Yesu kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.
Petro Amkana Yesu Tena
25 Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamwuliza, “Wewe ni mmoja wa wana funzi wake?” Petro akakana, akasema, “Mimi sio.” 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alim kata sikio, akamwuliza, “Je, sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 27 Kwa mara nyingine tena Petro akakataa kwamba alimfa hamu Yesu. Wakati huo huo jogoo akawika.
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
28 Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa wakampeleka kwenye ikulu ya gavana wa Kirumi. Ilikuwa ni alfa jiri. Wayahudi waliokuwa wanamshtaki Yesu hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa wachafu kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika sikukuu ya Pasaka. 29 Kwa hiyo Pilato akatoka nje kuwaona akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” 30 Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa ametenda maovu tusingemleta kwako.” 31 Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote.” 32 Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu atakavy okufa, yapate kutimia. 33 Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akam wita Yesu akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” 34 Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwe nyewe au kutokana na ulivyoambiwa kunihusu mimi?” 35 Pilato akamjibu, “Unadhani mimi ni Myahudi? Watu wa taifa lako na maku hani wao wakuu wamekushtaki kwangu. Umefanya kosa gani?” 36 Ndipo Yesu akamwambia, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Ingekuwa hivyo, watumishi wangu wangenipigania na kuhakikisha kuwa siwekwi mikononi mwa Wayahudi; lakini Ufalme wangu hautoki ulimwenguni.” 37 Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema mimi ni mfalme. Nimezaliwa na nime kuja ulimwenguni kwa makusudi ya kushuhudia kweli. Mtu ye yote anayepokea yaliyo ya kweli anakubaliana na mafundisho yangu.” 38 Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote ali lotenda mtu huyu.
39 Lakini kuna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachilie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mngependa nimwachilie huru huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?” ’ 40 Wao wakapiga kelele wakisema, “Hapana, usimwachilie huyo. Tufungulie Bar aba!” Baraba alikuwa mnyang’anyi.
Copyright © 1989 by Biblica