Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 17

Adhabu Ya Babiloni

17 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi. Wafalme wa dunia wamezini naye, na watu waishio duniani walilewa divai yake ya uzinzi.” Kisha nikiwa katika Roho malaika akanipeleka nyikani, nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumtukana Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu na kujipamba kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake. Na kwenye kipaji cha uso wake yaliandikwa maneno yenye maana iliyofichika: “Babiloni Mkuu, Mama wa Makahaba na wa Machukizo yote ya Duniani.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa damu ya watu wa Mungu na damu ya watu waliouawa kwa kumshuhudia Yesu. Nilipomwona, nilistaajabu sana. Lakini yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufunulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyembeba, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.

Jambo hili linahitaji hekima na maarifa. Vile vichwa saba ni milima saba ambapo huyo mwanamke ameketi. 10 Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao kati yao watano wamekwisha kuanguka, mmoja yupo na mmoja hajaja bado, naye akija, atalazimika kukaa kwa muda mfupi tu. 11 Na huyo mnyama aliyekuwapo ambaye hayupo, yeye ni wa nane, lakini ni wa kundi la wale saba naye pia ataan gamizwa.

12 Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawaja tawazwa bado, lakini watatawazwa kwa muda wa saa moja tu pamoja na yule mnyama. 13 Hawa wana nia moja nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14 Watampiga vita Mwana-Kondoo na Mwa na-Kondoo atawashinda kwa kuwa yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, na wale walio pamoja naye wanaitwa wateule na waami nifu.”

15 Kisha akaniambia, “Yale maji uliyoyaona alipokuwa amekaa yule kahaba, ni watu na umati wa watu na mataifa na lugha. 16 Na zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama watamchukia huyo kahaba; watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kabisa kwa moto. 17 Maana Mungu amefanya mioyo yao kutimiza mapenzi yake, kwa kuwafanya wawe na nia moja ya kumpa mamlaka yao ya kifalme huyo mnyama, mpaka maneno ya Mungu yataka potimizwa. 18 Na yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkuu wenye mamlaka juu ya wafalme wa dunia.”

Error: Book name not found: Zech for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 16

16 “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkapoteza imani yenu. Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu. Watu watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi. Lakini nimew aambia mambo haya kusudi muda huo utakapofika mkumbuke kuwa nili kuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.

Kazi Ya Roho Mtakatifu

“Lakini sasa ninakwenda kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ Kwa kuwa nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.

12 “Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia lakini hamwezi kuy apokea sasa. 13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.

Huzuni Na Furaha

16 “Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”

19 Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20 Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22 Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23 Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.

Ushindi

25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26 Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.” 29 Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32 Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami. 33 Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica