Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 11

Mashahidi Wawili

11 Ndipo nikapewa kipimo kama fimbo, nikaambiwa, “Nenda kapime Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu na uwahesabu watu waabuduo humo. Lakini usipime uwanja wa nje ya Hekalu, uache, kwa sababu uwanja huo wamepewa mataifa wasiomjua Mungu. Wao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Nami nitawapa uwezo mashahidi wangu wawili watoe unabii kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini na mbili, wakiwa wamevaa magunia.”

Manabii hao wawili ni ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana na mbele ya nchi yote. Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Na hivyo ndivyo atakavyokufa mtu ye yote atakayetaka kuwad huru. Watu hawa wanayo mamlaka ya kuyafunga mawingu ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Watakuwa na mamlaka juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuleta maafa ya kila aina ulimwenguni, kama wapendavyo. Lakini wakishamaliza kutoa unabii huo, yule mnyama atokaye katika shimo la kuzimu ata wapiga vita na kuwashinda na kuwaua. Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkuu ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo Bwana wao alisulubiwa. Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti zao, na hawataruhusu wazikwe. 10 Watu waishio duniani watafura hia kifo cha manabii hao wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu manabii hao waliwatesa watu waishio ulimwenguni.

11 Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu. 12 Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati maadui zao wakiwatazama. 13 Wakati huo huo, kukatokea tetemeko kuu la nchi, na sehemu moja ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo na waliosalimika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.

14 Maafa ya pili yamekwisha kupita. Lakini maafa ya tatu yanakuja upesi.

Tarumbeta Ya Saba

15 Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” 16 Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, 17 wakisema, “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi uli yeko na uliyekuwako; kwa kuwa umeuchukua uweza wako mkuu na ukaanza kutawala. 18 Watu wa mataifa walikasirika kwa kuwa wakati wa ghadhabu yako umefika. Wakati umefika wa kuwahukumu wafu na kuwapa tuzo watumishi wako manabii na watakatifu walioli tukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo; na wakati umefika wa kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa na sanduku la agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo na tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.

Error: Book name not found: Zech for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 10

Mchungaji Mwema

10 “Ninawaambia hakika, mtu asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya ndani kwa kupitia njia nyin gine, ni mwizi na mnyang’anyi. Anayepitia mlangoni ndiye mchun gaji wa kondoo. Mlinzi humfungulia mlango na kondoo hutambua sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza nje ya zizi. Akiisha watoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaifahamu sauti yake. Kondoo hawam fuati mtu wasiyemfahamu bali humkimbia, kwa sababu hawatambui sauti ya mgeni.” Yesu alitumia mfano huu lakini wao hawakuel ewa maana yake.

Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili. 11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.

14 Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15 kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”

19 Maneno haya yalisababisha mafarakano tena kati ya Way ahudi. 20 Wengi wao walisema, “Huyu amepagawa na shetani, kwa nini tuendelee kumsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na shetani. Je, shetani anaweza kumpo nya kipofu?”

Yesu Anajitambulisha

22 Ilikuwa sikukuu ya Utakaso wa Hekalu wakati wa majira ya baridi, 23 na Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24 Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26 Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”

31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”

Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”

34 Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35 Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38 lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”

39 Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.

40 Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 Na wengi wakamwamini Yesu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica