Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 4

Kiti Cha Enzi Kilichoko Mbinguni

Baada ya hayo nilitazama, nikaona mlango ulio wazi mbin guni. Na ile sauti niliyokuwa nimeisikia ikisema nami kama tar umbeta ikasema, “Njoo huku juu nami nitakuonyesha yatakayotokea baada ya haya. ” Ghafla nilikuwa katika Roho, na mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa. Aliyeketi kwenye kiti hicho cha enzi alionekana kama jiwe zuri jekundu na akiki, na upinde wa mvua ulizunguka kile kiti cha enzi, ukione kana kama zumaridi. Kiti hicho kilizungukwa na viti vingine ishirini na vinne vya enzi ambavyo juu yake walikaa wazee ishi rini na wanne waliokuwa wamevalia mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani. Na katika kile kiti cha enzi kulitoka umeme, ngurumo na sauti. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya kile kiti cha enzi, ambazo ni zile roho saba za Mungu. Mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na kitu kinachofanana na bahari ya kioo iking’aa kama jiwe la kioo. Katikati, kuzunguka kile kiti cha enzi, walikuwapo viumbe hai wanne, wenye macho kila mahali, mbele na nyuma.

Kiumbe hai wa kwanza alifanana na simba, wa pili alifanana na ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, wa nne alifanana na tai arukaye. Na hawa viumbe hai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita na macho kila mahali, hata chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kuimba, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

Kila mara viumbe hao wanne walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na aishie milele na milele, 10 wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wakaziweka taji zao mbele ya kile kiti cha enzi wakisema, 11 “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”

Error: Book name not found: Hag for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 3

Nikodemo Amwendea Yesu Usiku

Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo, alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”

Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”

Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”

Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10 Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli na huyaelewi mambo haya? 11 Ninakwambia kweli, sisi tunazungumza lile tunalo lijua na tunawashuhudia lile tuliloliona, lakini hamtaki kutu amini! 12 Ikiwa hamuniamini ninapowaambia mambo ya duniani, mtaniaminije nitakapowaambia habari za mbinguni? 13 Hakuna mtu ye yote ambaye amewahi kwenda juu mbinguni isipokuwa mimi Mwana wa Adamu niliyeshuka kutoka mbinguni. 14 Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu 15 ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele . 16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20 Kwa kuwa kila mtu atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini kila mtu anayeishi maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo yake yanatokana na utii kwa Mungu.”

Yesu Na Yohana Mbatizaji

22 Baadaye, Yesu alikwenda katika jimbo la Yudea pamoja na wanafunzi wake akakaa nao kwa muda na pia akabatiza watu. 23 Yohana naye alikuwa akibatiza watu huko Ainoni karibu na Sal imu kwa sababu huko kulikuwa na maji mengi. Watu walikuwa wakim fuata huko naye akawabatiza. 24 Wakati huo Yohana alikuwa bado hajafungwa gerezani.

25 Ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kadhaa wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu swala la kutawadha. 26 Basi wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe nga’mbo ya pili ya mto wa Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27 Yohana akawa jibu, “Mtu hawezi kuwa na kitu kama hakupewa na Mungu. 28 Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema mimi si Kristo ila nimetumwa nimtangulie. 29 Bibi harusi ni wa bwana harusi. Lakini rafiki yake bwana harusi anayesimama karibu na kusikiliza, hufu rahi aisikiapo sauti ya bwana harusi. Sasa furaha yangu imekamil ika. 30 Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi niwe mdogo zaidi.”

Aliyetoka Mbinguni

31 “Yeye aliyekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. Anayetoka duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya hapa duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya watu wote. 32 Anayashuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia lakini hakuna anayekubali maneno yake. 33 Lakini ye yote anayekubali maneno yake, anathibitisha kwamba aliyosema Mungu ni kweli. 34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu kwa maana Mungu amempa Roho wake pasipo kipimo. 35 Baba anampenda Mwanae na amempa mam laka juu ya vitu vyote. 36 Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica