M’Cheyne Bible Reading Plan
Ujumbe Kwa Kanisa La Sardi
3 “Kwa malaika wa Kanisa la Sardi andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako; na kwamba una sifa ya kuwa hai, na kumbe umekufa. 2 Amka! Imarisha kilichobakia kabla hakijaharibika kabisa, kwa maana nimeona kwamba kazi zako hazijakamilika mbele za Mungu wangu. 3 Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala huta jua saa nitakayokujia.
4 Bado wako watu wachache huko Sardi ambao hawajachafua mavazi yao. Wao watatembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi yao meupe kwa maana wanastahili. 5 Atakayeshinda atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake katika kitabu cha uzima bali nitalikiri jina lake mbele ya Baba yangu na mbele za malaika wake.
6 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anayaam bia makanisa.”’
Ujumbe Kwa Kanisa La Filadelfia
7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, na anachoki funga hakuna awezaye kukifungua.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango ulio wazi ambao hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba ingawa nguvu yako ni ndogo lakini umelishika neno langu na hujalikana jina langu. 9 Sikiliza, wale watu ambao ni wa sinagogi la she tani, wale wajiitao Wayahudi kumbe sio, bali ni waongo; nitawafa nya waje wapige magoti mbele yako na wakiri kwamba nimekupenda. 10 Kwa kuwa umeshika agizo langu la kustahimili kwa subira, nitakulinda wakati wa ile dhiki itakayokuja duniani pote kuwajar ibu waishio ulimwenguni.
11 Ninakuja upesi. Shika sana kile ulicho nacho asije mtu akachukua taji yako. 12 Atakayeshinda nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo kamwe. Na nitaan dika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wake Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unakuja kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika juu yake jina langu jipya.
13 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Laodikia
14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa vyote alivyoumba Mungu.
15 Nayajua matendo yako; kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali kama ungalikuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa kuwa wewe ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 17 Unajigamba ukisema, ‘Mimi ni tajiri , nimefanikiwa wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, maskini, kipofu; tena wewe ni uchi. 18 Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona.
19 Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako. 20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 22 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Yesu Ahudhuria Harusi Mjini Kana
2 Siku ya tatu kulikuwa na harusi katika mji wa Kana ulioko Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo 2 na Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa pia. 3 Divai ilipowaishia, mama yake Yesu alimwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akamjibu, “Mama, mbona unanihusisha kwenye jambo hili? Wakati wangu bado haujafika.” 5 Mama yake akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni. ” 6 Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu.
Imekuwaje wewe ukaiweka divai nzuri mpaka sasa?”
11 Hii ilikuwa ishara ya kwanza aliyofanya Yesu. Muujiza huu ulifanyika katika mji wa Kana huko Galilaya, ambako Yesu alidhi hirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya haya, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walikwenda Kapernaumu ambapo alikaa kwa siku chache.
Yesu Alitakasa Hekalu
13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”
18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”
20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku tatu?”
21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno ali yosema Yesu.
23 Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara za ajabu alizokuwa akifanya, wakamwamini. 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua binadamu wote. 25 Hakuhitaji mtu ye yote amwambie lo lote kuhusu bina damu. Alijua yote yaliyokuwa mioyoni mwao.
Copyright © 1989 by Biblica