M’Cheyne Bible Reading Plan
Ujumbe Kwa Kanisa La Efeso
2 “Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: ‘Haya ni maneno ya yule aliyeshika nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. 2 Najua matendo yako, bidii yako na uvumilivu wako. Najua kuwa huwezi kuvumilia watu waovu na kwamba umewapima wale wanaojiita mitume na kumbe sio, na umetambua ya kuwa wao ni waongo. 3 Najua umevumilia na kustahimili mateso kwa ajili ya jina langu, wala hujachoka .
4 Lakini nina neno hili juu yako: kwamba umeacha upendo wako wa kwanza. 5 Kumbuka pale ulipokuwa kabla ya kuanguka. Tubu, uache dhambi zako, ukafanye matendo ya mwanzo. Kama hukuacha dhambi zako, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. 6 Lakini una jambo moja zuri: unayachukia matendo ya Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
7 Mwenye nia ya kusikia na ayasikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa . Atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ambao uko katika bustani ya Mungu.”’
Ujumbe Kwa Kanisa La Smirna
8 “Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye wa kwanza na wa mwisho; aliyekufa kisha akawa hai tena.
9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri! Najua matukano wanayokutukana wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi; wao ni sinagogi la shetani. 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuhakikishia kuwa shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu. Nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
11 Mwenye nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa. Atakayeshinda hatadhuriwa na kifo cha pili.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Pergamo
12 “Kwa malaika wa Kanisa la Pergamo andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili.
13 Ninajua unakoishi, kule ambako shetani ameweka kiti chake cha enzi. Hata hivyo umelishika jina langu, wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambao ni maskani ya shetani.
14 Lakini nina mambo machache juu yako: baadhi yenu ni wafu asi wa mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki awashaw ishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na kufanya uasherati. 15 Na tena baadhi yenu wanafu ata mafundisho ya Wanikolai. 16 Basi tubuni mwache dhambi zenu: ama sivyo nitakuja hivi karibuni na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
17 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho ana waambia makanisa. Atakayeshinda nitampa sehemu ya ile mana iliy ofichwa, nami nitampa jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.’
Ujumbe Kwa Kanisa La Thiatira
18 “Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika hivi: ‘Haya ni maneno ya Mwana wa Mungu ambaye macho yake ni kama moto uwakao, na miguu yake inang’aa kama shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na subira yako; na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya mwanzo.
20 Hata hivyo ninalo jambo hili juu yako: unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kwa miungu. 21 Nimempa muda atubu, aache uasher ati, lakini hataki kutubu. 22 Kwa hiyo nitamtupa kitandani kwa ugonjwa, na atapata mateso makali pamoja na hao wanaozini naye wasipotubu matendo yake. 23 Tena nitawaua watoto wake. Ndipo makanisa yote yatajua kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na akili za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini ninawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamfuati mafundisho ya Yezebeli, wala ham kujifunza hayo wengine wanayoyaita ‘siri za ndani’ za shetani, sitawaongezea mzigo mwingine. 25 Bali mshike sana hicho mlicho nacho mpaka nitakapokuja.
26 Atakayeshinda na kuendelea kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa. 27 ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunja vipande vipande kama chombo cha udongo 28 Pia nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaambia makanisa.’ ”
Neno Alifanyika Mwili
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: “Huyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu.
Ujumbe Wa Yohana Mbatizaji
19 Viongozi wa Wayahudi waliwatuma makuhani na Walawi wakam wulize Yohana, “Wewe ni nani?” 20 Yohana akawajibu wazi wazi pasipo kuficha, “Mimi siye Kristo.” 21 Wakamwuliza, “Wewe ni nani basi? Wewe ni Eliya ?” Akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.” 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Tueleze, wewe hasa ni nani?”
23 Akawajibu kwa kutumia maneno ya nabii Isaya, “Mimi ni sauti ya mtu anayeita kwa sauti kuu nyikani, ‘Nyoosheni njia ata kayopita Bwana.”’ 24 Baadhi ya wale waliotumwa na Mafarisayo 25 walimwuliza, “Kama wewe si Kristo, wala Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini unabatiza watu?”
26 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua. 27 Yeye anakuja baada yangu, lakini mimi sistahili hata kumvua viatu vyake.”
28 Mambo haya yalitokea Bethania, kijiji kilichoko ng’ambo mashariki ya mto wa Yordani, ambapo Yohana alikuwa akibatiza watu.
Mwana Kondoo Wa Mungu
29 Kesho yake Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazameni! Huyu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwapo kabla sijazaliwa.’ 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini nimekuja nikibatiza kwa maji kusudi apate kufahamika kwa watu wa Israeli.”
32 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akish uka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 Mimi nisingem tambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji ali kuwa ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 Mimi nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”
Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu
35 Kesho yake, Yohana alikuwapo pale pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesu akipita, alisema, “Tazameni! Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, walimfuata Yesu. 38 Yesu akageuka akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Rabi’ 39 Yesu akawajibu, “Njooni mkapaone!” Ilikuwa yapata saa kumi jioni. Basi wakaenda wakaona alipokuwa anaishi, wakashinda naye siku hiyo.
40 Mmojawapo wa hao wanafunzi wawili waliomfuata Yesu baada ya kusikia maneno ya Yohana, alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro. 41 Mara baada ya haya Andrea alikwenda kumtafuta ndugu yake akamwambia, “Tumemwona Masihi,” yaani Kristo. 42 Andrea akampeleka Simoni kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana; sasa utaitwa Kefa.” Tafsiri ya Kefa kwa Kigiriki ni Petro, maana yake ‘Mwamba’.
Yesu Anawaita Filipo Na Nathanaeli
43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akakutana na Filipo, akamwambia, “Nifuate.” 44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji ambapo Andrea na Petro walikuwa wanaishi. 45 Fil ipo naye akamtafuta Nathanaeli akamwambia, “Tumekutana na Yesu wa Nazareti mwana wa Yusufu, ambaye Musa katika Torati na pia Manabii waliandika habari zake.” 46 Nathanaeli akajibu, “Je, inawezekana kitu cho chote chema kikatoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo ukajionee mwenyewe.” 47 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akasema, “Huyu ni Mwisraeli halisi. Hana udanganyifu wo wote.” 48 Nathanaeli akamwuliza, “Umenifaha muje? ” Yesu akamjibu, “Nilikuona wakati ulipokuwa chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” 49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nimekuambia kwamba nili kuona chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo!” 51 Ndipo akawaambia, “Ninawaambia hakika, mtaona mbingu ikifunguka, na malaika wa Mungu wakienda mbinguni na kushuka juu yangu mimi Mwana wa Adamu.”
Copyright © 1989 by Biblica