Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Yohana 4

Kujihadhari Na Maadui Wa Kristo

Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani. Na hivi ndivyo mtakavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayokiri kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwana damu, hiyo inatoka kwa Mungu. Lakini roho yo yote ambayo haim kiri Kristo, si ya Mungu. Hii ndio roho ya mpinga-Kristo, ambayo mmekwisha kusikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko duniani.

Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda; kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani. Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanayoyasema ni ya ulimwengu na watu wa dunia huwasikiliza. Sisi ni wa Mungu. Anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiye wa Mungu hatusikilizi. Na hivi ndivyo tunaweza kutambua kati ya Roho wa kweli na roho wa uongo.

Mungu Ni Upendo

Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.

Error: Book name not found: Nah for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 19

19 Yesu akaingia Yeriko, akiwa safarini kuelekea Yerusalemu. Hapo, alikuwapo mtu mmoja mkuu wa watoza kodi na pia mtu tajiri, jina lake Zakayo. Yeye alitamani sana kumwona Yesu lakini hakuweza kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, naye alikuwa mfupi sana. Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu ambaye angepitia njia ile. Yesu alipofika chini ya huo mkuyu, akatazama juu akamwambia: “Zakayo! Shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” Mara moja Zakayo akashuka, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. Watu wote waliokuwepo, wakaanza kunung’unika, “Amekwenda kuwa mgeni nyumbani kwa mwenye dhambi!” Lakini Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Sikia Bwana, nusu ya mali yangu ninaitoa hivi sasa niwagawie maskini, na kama nimemdhulumu mtu ye yote, nitamrudishia mara nne zaidi.” Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. 10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”

Mfano Wa Fedha

11 Wakati walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu aliendelea kuwaambia mfano. Wakati huo watu walikuwa wakidhani kwamba kwa kuwa walikuwa wanakaribia Yerusalemu, Ufalme wa Mungu ungetokea mara. 12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’ 14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’ 15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.

16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’ 17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’

18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ 19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ 20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’

22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda; 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’ 24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’

Yesu Aingia Yerusalemu

28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu. 29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’

32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana- punda wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” 35 Wakamleta kwa Yesu. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Alipokuwa akienda, watu wakatan daza nguo zao barabarani. 37 Alipokaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote wa wanafunzi wake wakaanza kwa sauti kuu kumsifu Mungu kwa furaha kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona Yesu akifanya, 38 wakasema: “Amebarikiwa Mfalme anayekuja kwa jina la Bwana! Amani mbinguni na Utukufu kwa Mungu.” 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo katika umati wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.” 40 Yesu akawajibu, “Nawaambia, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”

Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu

41 Alipokaribia Yerusalemu, akauona mji, aliulilia,

42 akasema, “Laiti ungalijua leo jinsi ya kupata amani! Lakini sasa huoni! 43 Kuna siku ambapo maadui zako watakuzungushia ukuta na kukuzingira na kukushambulia kutoka kila upande. 44 Watakutupa chini wewe na wanao ndani ya kuta zako na hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine. Hii ni kwa sababu hukutaka kutambua wakati

Yesu Aingia Hekaluni

45 Ndipo akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale wal iokuwa wakifanya biashara humo. 46 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.’ Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”

47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua 48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica