M’Cheyne Bible Reading Plan
Upendo Na Utii
2 Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye mtetezi wetu kwa Baba, yaani Yesu Kristo mwenye haki. 2 Kristo ndiye sadaka iliyotolewa kwa ajili ya dhambi zetu, na wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.
3 Na tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua Kristo ikiwa tunatii amri zake. 4 Mtu ye yote akisema, “Ninamjua’ 5 Lakini mtu ye yote anayetii neno lake, huyo ndiye ambaye upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kwa kweli. Hivi ndivyo tunavy ojua kuwa tumo ndani ya Kristo. 6 Mtu anayesema anadumu ndani ya Kristo anapaswa kuishi kama Yesu Kristo mwenyewe alivyoishi.
7 Wapendwa, siwaandikii amri mpya bali amri ile ambayo mme kuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilok wisha kusikia. 8 Lakini hata hivyo amri hii ninayowaandikieni ni mpya; ambayo ukweli wake unaonekana kwake na kwenu, kwa sababu giza linatoweka na nuru ya kweli imekwishaanza kuangaza. 9 Mtu anayesema kwamba anaishi nuruni, naye anamchukia ndugu yake, bado yumo gizani. 10 Anayempenda ndugu yake anaishi katika nuru na wala hana kitu cha kumfanya ajikwae. 11 Lakini anayemchukia ndugu yake anaishi gizani na anatembea gizani, wala hajui aen dako, kwa sababu giza limempofusha macho.
Kwa Watoto, Baba Na Vijana
12 Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Ninawaandikieni ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Ninawandikieni ninyi watoto, kwa kuwa mmemjua Baba. 14 Ninawaan dikieni ninyi akina baba, kwa kuwa mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Msipende Dunia
15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni. 17 Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.
Onyo Kuhusu Adui Wa Kristo
18 Watoto wapendwa, huu ni wakati wa mwisho. Na kama mlivy okwisha kusikia kwamba yule mpinga-Kristo anakuja, hata sasa wapinga-Kristo wengi wamekwisha kuja. Kwa hiyo tunajua kuwa huu ni wakati wa mwisho. 19 Watu hao walitoka kati yetu, lakini hawakuwa wa kundi letu. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangeende lea kuishi pamoja nasi; lakini waliondoka ili iwe wazi kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kundi letu.
20 Lakini ninyi mmemiminiwa Roho Mtakatifu na nyote mnaijua kweli. 21 Siwaandikii hivi kwa kuwa hamuijui kweli bali kwa sababu mnaijua na kwa kuwa hakuna uongo utokao katika kweli. 22 Je, mwongo ni nani? Mwongo ni yule anayekana kwamba Yesu si Kristo. Mtu huyo ndiye mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Mtu anayemkana Mwana hawezi kumjua Baba; mtu anayemkiri Mwana anamjua na Baba pia.
24 Hakikisheni kwamba ujumbe mliosikia tangu mwanzo unadumu mioyoni mwenu. Ujumbe huo ukikaa mioyoni mwenu, ninyi pia mtadumu ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na yeye ametuahidi uzima wa milele.
26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale wanaojaribu kuwapo tosha. 27 Lakini yule Roho Mtakatifu mliyempokea anakaa ndani yenu wala hamhitaji mtu kuwafundisha. Lakini kama vile huyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha mambo yote, naye ni wa kweli wala si wa uongo; kama alivyowafundisha, dumuni ndani yake.
Watoto Wa Mungu
28 Na sasa, wanangu, kaeni siku zote ndani yake, kusudi ata kapotokea tuwe na ujasiri na wala tusijitenge naye kwa kuona aibu atakapokuja.
29 Kama mnajua kwamba yeye ni wa haki, basi mnajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.
17 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Majaribu yanayowafanya watu watende dhambi hayana budi kuwepo. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. 2 Ingekuwa nafuu kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito shingoni na kuzamishwa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. 3 Kwa hiyo, jihadharini. Ndugu yako akikukosea mwonye; akiomba msamaha, msamehe. 4 Hata kama akikuko sea mara saba kwa siku na kila mara aje kwako akisema, ‘Nisa mehe
5 Wanafunzi wakamwambia Bwana, “Tuzidishie imani.” 6 Aka waambia, “Kama mngekuwa na imani kiasi cha punje ndogo sana ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu, ‘Ng’oka na mizizi yote ukaote baharini,’ nao ungewatii!”
Wajibu Wa Mtumishi
7 “Tuseme mmoja wenu ana mtumishi aliyekwenda shambani kulima au kuchunga kondoo. Je, mtumishi huyo akirudi utamwambia, ‘Karibu keti ule chakula’? 8 Hata kidogo. Badala yake utamwambia, ‘Nitayarishie chakula na ujiandae kunihudumia ninapokula na kunywa, na baada ya hapo unaweza kula chakula chako.’ 9 Wala hutamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza wajibu wake. 10 Hali kadhalika nanyi, baada ya kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi ni watumishi tusiostahili, tumetimiza wajibu wetu tu.”’
Yesu Atakasa Wakoma Kumi
11 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu alipitia kati ya Samaria na Galilaya. 12 Alipokuwa akikaribia kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye. 13 Wakasimama mbali wakaita kwa nguvu, “Yesu! Bwana! tuonee huruma!” 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Na walipokuwa wakienda, wakapona ukoma wao. 15 Mmoja wao alipoona kwamba ame pona, akarudi kwa Yesu akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16 Kwa heshima kubwa akajitupa miguuni kwa Yesu akamshukuru. Yeye ali kuwa ni Msamaria .
17 Yesu akauliza, “Hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale tisa wengine? 18 Hakuna hata mmoja aliyekumbuka kurudi kumsifu Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 19 Akamwambia, “Inuka, uende; imani yako imekuponya.” Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja
20 Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa’ au ‘Ule kule’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona siku yangu moja, mimi Mwana wa Adamu lakini ham taiona. 23 Watu watawaambia, ‘Yule pale’ au, ‘Huyu hapa!’ Msiwa kimbilie. 24 Kwa maana kama umeme unavyomulika mbingu kutoka upande mmoja hadi mwingine, ndivyo itakavyokuwa siku ya kuja kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 25 Lakini kwanza itanipasa nite seke sana na kukataliwa na watu wa kizazi hiki. 26 Kama ilivy okuwa nyakati za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku ya kurudi kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 27 Wakati wa Nuhu watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo mafuriko yakaja yakawaangamiza wote. 28 Hata nyakati za Lutu ilikuwa hivyo hivyo. Watu walikuwa wakila, waki nywa, wakifanya biashara, wakilima na kujenga. 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, moto ulishuka kutoka mbinguni uka waangamiza wote. 30 Ndivyo itakavyokuwa siku ambapo mimi Mwana wa Adamu nitakapotokea kwa utukufu.
31 “Siku hiyo, mtu akiwa darini na vitu vyake vikiwa ndani, asiteremke kuvichukua. Hali kadhalika atakayekuwa shambani asi rudi nyumbani kuchukua cho chote. 32 Kumbukeni yaliyompata mke wa Lutu! 33 Mtu ye yote anayejaribu kusalimisha maisha yake atayapoteza; na ye yote atakayekuwa tayari kuyapoteza maisha yake atayaokoa. 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 35 Wana wake wawili watakuwa wanatwanga pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” [ 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.] 37 Wakamwuliza, “Haya yatatokea wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai wanapokutanika.” Mfano Wa Hakimu Dhalimu
Copyright © 1989 by Biblica