M’Cheyne Bible Reading Plan
Walimu Wa Uongo
2 Lakini pia walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyotokea walimu wa uongo kati yenu. Kwa siri, watain giza mafundisho ya upotovu hata kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watajiletea maangamizi ya haraka. 2 Na wengi wata fuata tamaa zao potovu, na kwa ajili ya matendo yao njia ya kweli itadharauliwa. 3 Nao katika tamaa yao watajaribu kuwanunua kwa kuwaambia hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu yao imekuwa tayari tangu zamani, wala mwangamizi wao hajalala usingizi.
4 Maana kama Mungu hakuwahurumia malaika walipotenda dhambi bali aliwatupa kuzimu, katika vifungo vya giza wakae huko mpaka siku ya hukumu; 5 kama hakuuhurumia ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomcha Mungu, akamlinda Noe mjumbe wa haki, pamoja na watu saba wengine; 6 kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza ikawa majivu, akaifanya kuwa mfano kwa wote ambao hawatamcha Mungu; 7 na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki ambaye alihuzunishwa na maisha ya uchafu ya watu wahalifu - 8 kwa sababu yale maasi aliyoona na kusikia huyo mtu wa Mungu alipoishi kati yao yalimhuzunisha usiku na mchana - 9 basi ikiwa ni hivyo, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wa Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika hali ya adhabu mpaka siku ya hukumu. 10 Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa chafu za mwili na kudharau mamlaka. Watu hawa ni shupavu na katika kiburi chao, hawaogopi kuwatu kana viumbe vitukufu wa mbinguni;
11 ingawa hata malaika, ambao wana nguvu na uwezo zaidi, hawawashtaki au kuwatukana viumbe hao mbele za Bwana. 12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiy oyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawal iwa na hisia za mwili, ambao wamezaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa, na kama wanyama, wao pia wataangamizwa.
13 Watalipizwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Furaha yao ni kufanya karamu za ufisadi mchana, wazi wazi. Wao huleta aibu na fedheha wanaposhiriki katika karamu zenu kwa kuwa wakati wote huo, wanajifurahisha katika upotevu wao. 14 Macho yao yamejaa uzinzi, nao hutenda dhambi bila kikomo. Huwahadaa watu dhaifu. Mioyo yao imezoea kutamani. Hawa ni wana wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa kupata fedha kwa kufa nya maovu. 16 Balaamu alikaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena kwa sauti ya binadamu akamzuia huyo nabii asiendelee na kichaa chake.
17 Watu hawa ni kama chemchemi zilizokauka na ukungu upeper ushwao na tufani, na lile giza jeusi limewekwa tayari kwa ajili yao. 18 Wao hutamka maneno matupu ya majivuno na kutumia tamaa mbaya za mwili kuwanasa tena wale ambao ndio kwanza wameepukana na watu wanaoishi maisha ya uovu. 19 Huwaahidi hao waliowanasa kuwa watakuwa huru kabisa, lakini wao wenyewe ni watumwa wa upo tovu. Kwa maana mtu huwa mtumwa wa kitu kile kinachomshinda nguvu. 20 Kwa maana wale waliokwisha kuponyoka kutoka katika uchafu wa dunia hii kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo , kisha wakanaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. 21 Ingekuwa heri kwao kama hawa kuijua kamwe njia ya haki, kuliko kuifahamu kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyopewa. 22 Kama methali moja isemavyo, “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine, “Nguruwe huoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni.”
14 Siku moja ya sabato Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimtazama kwa makini. 2 Mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba miguu na mikono akaja mbele yake. 3 Yesu akawauliza walimu wa sheria na Mafari sayo, “Je, sheria inaruhusu kumponya mtu siku ya sabato au hairuhusu?” 4 Wakakaa kimya. Basi Yesu akamshika yule mgonjwa akamponya, akamruhusu aende zake. 5 Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake ambaye ametumbukia katika kisima siku ya sabato, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” 6 Hawakuwa na la kujibu.
7 Alipoona jinsi wageni walioalikwa walivyokuwa wakichagua viti vya wageni wa heshima, akawaambia mfano huu: 8 “Mtu akiku alika harusini, usikae kwenye kiti cha mgeni wa heshima. Inaweze kana kuwa amealika mheshimiwa akuzidiye, 9 na yule aliyewaalika ninyi wawili akaja kukuambia, ‘Tafadhali mpishe huyu bwana.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kwenda kukaa katika kiti cha nyuma kabisa. 10 Badala yake, unapoalikwa, chagua kiti cha nyuma; na mwenyeji wako akikuona atakuja akuambie, ‘Rafiki yangu, njoo kwe nye nafasi ya mbele zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wote. 11 Kwa maana kila mtu anayejitukuza atash ushwa naye ajishushaye atatukuzwa.”
12 Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo kar amu ya chakula cha mchana au jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako tajiri; ukifanya hivyo wao nao watakualika kwao na hivyo utakuwa umelipwa kwa kuwaalika. 13 Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu; 14 nawe utapata baraka kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa.
Mfano Wa Karamu Ya Ufalme Wa Mbinguni
15 Mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja naye aliposikia maneno haya akamwambia, “Ana heri mtu atakayepata nafasi ya kula katika karamu ya Ufalme wa Mbinguni!” 16 Yesu akamjibu, ‘ ‘Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 17 Wakati wa sherehe ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaam bie walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ni tayari sasa.’ 18 Lakini wote, mmoja mmoja, wakaanza kutoa udhuru. Wa kwanza akasema, ‘ Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ 19 Mwingine akasema, ‘Nimenunua ng’ombe wa kulimia, jozi tano; nimo njiani kwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 20 Na mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’
21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’
22 “Baadaye yule mtumishi akamwambia ‘Bwana, yale uliyon iagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ 23 Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na njia zilizoko nje ya mji uwalazimishe watu waje mpaka nafasi zote zijae. 24 Ninawaambia, hakuna hata mmoja wa wale niliowapelekea mwaliko rasmi atakayeionja karamu yangu.”
Gharama Ya Kuwa Mfuasi Wa Yesu
25 Wakati mmoja umati mkubwa wa watu ulipokuwa ukifuatana na Yesu, yeye aligeuka, akawaambia, 26 “Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mfuasi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, kaka zake na dada zake; naam, hata maisha yake mwenyewe. 27 Na ye yote asiyebeba msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mfuasi wangu.
28 “Ni nani kati yenu ambaye kama anataka kujenga, hatakaa kwanza na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha ujenzi? 29 Kwa maana ikiwa atajenga msingi halafu ashindwe kuendelea, wote watakaouona watamcheka 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini ameshindwa kumal iza!’
31 “Au tuseme mfalme mmoja anataka kwenda vitani kupigana na mfalme mwingine: si atakaa kwanza ajishauri kama yeye na jeshi lake lenye watu elfu kumi ataweza kupigana na yule anayekuja na watu elfu ishirini? 32 Kama hawezi, basi itambidi apeleke wajumbe wakati yule mfalme mwingine bado yuko mbali na kuomba masharti ya amani. 33 Hali kadhalika, hakuna mtu atakayeweza kuwa mfuasi wangu kama hataacha vyote alivyo navyo.”
Chumvi Isiyofaa
34 “Chumvi ni kitu kizuri. Lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, haiwezi kuwa chumvi tena. 35 Haifai kuwa udongo wala kuwa mbolea; watu huitupa nje. Mwenye nia ya kusikia na asikie!” Mfano Wa Kondoo Aliyepotea
Copyright © 1989 by Biblica