M’Cheyne Bible Reading Plan
Mafundisho Kwa Wake Na Waume
3 Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno 2 kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.
3 Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4 Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. 5 Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. 6 Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.
7 Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
Msilipe Ovu Kwa Ovu
8 Hatimaye, ninyi nyote muwe na nia moja, mhurumiane, mpen dane kama ndugu, muwe na mioyo ya upole na ya unyenyekevu. 9 Msi lipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; ila barikini kwa maana hili ndilo mliloitiwa na Mungu, mpate kurithi baraka. 10 Kwa maana, “Mtu anayependa kufurahia maisha, na anayetamani kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isi seme uongo. 11 Mtu huyo aepuke maovu, na atende mema; atafute amani na kuifuatilia sana. 12 Kwa maana macho ya Bwana huwaele kea wenye haki, na masikio yake husikiliza sala zao. Bali Bwana huwapa kisogo watenda maovu.”
Kuvumilia Mateso
13 Basi, ni nani atakayewadhuru ikiwa mna juhudi katika kutenda mema? 14 Lakini hata kama mtateseka kwa ajili ya haki, mtabarikiwa. Msiogope vitisho vyao wala msiwe na wasiwasi, 15 bali mioyoni mwenu mtukuzeni Kristo Bwana. Kila wakati muwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa unyenyekevu.
16 Dhamiri zenu ziwe safi ili mnapotukanwa, hao wanaotukana mwenendo wenu mwema katika Kristo, waone haya. 17 Maana ni afad hali kupata mateso kwa kutenda mema kama hayo ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 18 Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19 Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. 20 Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji. 21 Maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi, si kwa kuondoa uchafu kwenye miili yenu, bali kama dhamana ya kuwa na dhamiri njema kwa Mungu kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu Kristo. 22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.
10 Baada ya hayo, Yesu akawachagua wafuasi wengine sabini na wawili akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi lakini wafanya kazi ni wachache, kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno awapeleke wavunaji zaidi katika shamba lake. 3 Haya, nendeni. Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. 4 Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu; na msipoteze muda kumsalimu mtu ye yote njiani. 5 Mkiingia nyumba yo yote kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 6 Kama aishiye humo ni mwenye kupenda amani basi baraka hiyo itakaa naye, la sivyo, itawarudia. 7 Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa kile watakachowapa kwa sababu kila mfany akazi anastahili kulipwa mshahara. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. 8 Mkienda katika mji mkapokelewa: kuleni mtakachoandal iwa; 9 waponyeni wagonjwa na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu.’
10 “Lakini mkiingia katika mji msikaribishwe, nendeni katika mitaa yake mkaseme: 11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12 “Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13 Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto. 14 Lakini siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko kwenu. 15 Na ninyi je, watu wa Kapernaumu, mnafikiri mtainuliwa juu hadi mbinguni? La, Mungu atawatupa chini hadi kuzimuni. 16 “Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.”
17 Wale wanafunzi sabini na wawili wakarudi wakiwa na furaha. Wakamwambia Yesu, “Bwana, tukilitumia jina lako, hata pepo wanatutii!” 18 Akawajibu, “Nimemwona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni. 19 Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru. 20 Lakini msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, ila furahini kwa kuwa majina yenu yamean dikwa mbinguni.”
21 Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba. 22 Baba yangu amenika bidhi mambo yote. Hakuna anayemfahamu Mwana isipokuwa Baba: na hakuna anayemfahamu Baba isipokuwa Mwana na wale ambao Mwana ame penda humdhihirisha Baba kwao.” 23 Basi Yesu akawageukia wana funzi wake akawaambia faraghani, “Mmebarikiwa kuona mambo haya mnayoyaona! 24 Nawaambie ni kweli, manabii wengi na wafalme wal itamani kuona mnayoyaona na kusikia mnayoyasikia lakini hawaku pata nafasi hiyo.” Mfano Wa Msamaria Mwema
25 Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26 Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28 Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29 Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31 litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32 Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.
33 “Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34 akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35 Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.
36 “Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”
37 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38 Wakati Yesu na Wanafunzi wake walipokuwa wakiendelea na safari yao ya kwenda Yerusalemu, walifika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha Yesu nyum bani kwake. 39 Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Mariamu ambaye aliketi chini karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote. Kwa hiyo alikuja kwa Yesu akalalamika, “Bwana, hujali kwamba mdogo wangu ameniachia kazi zote? Mwambie aje anisaidie!” 41 Bwana akamjibu, “Martha! Martha! Mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42 Unahitaji kujua kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kil icho bora, na hakuna mtu atakayemnyang’anya.” Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake Kuomba
Copyright © 1989 by Biblica