M’Cheyne Bible Reading Plan
Onyo Kuhusu Upendeleo
2 Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. 2 Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. 3 Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,” 4 je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu?
5 Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa: je, Mungu hakuwachagua wale walio fukara hapa duniani kuwa matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidi wale wampendao? 6 Lakini ninyi mmemvunjia heshima aliye fukara. Je, si matajiri ndio wanaowagandamiza na kuwapelekeni mahakamani? 7 Je, si wao wanaolikufuru jina lile jema mliloitiwa? 8 Kama kweli mnatimiza ile sheria ya kifalme iliyomo katika Maandiko, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe,” mnafanya vema. 9 Lakini kama mnafanya ubaguzi, mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10 Kwa maana mtu ye yote anayetimiza sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini” ndiye huyo huyo aliyesema, “Usiue.” Kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria yote.
12 Kwa hiyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwa mtu asi yekuwa na huruma. Lakini huruma huishinda hukumu.
Imani Na Matendo
14 Kuna faida gani, ndugu zangu, ikiwa mtu atasema, “Ninayo imani,” na huku hana matendo? 15 Tuseme ndugu fulani au dada hana nguo wala chakula. 16 Ikiwa mmoja wenu atawaambia, “Nendeni salama, mkaote moto na kushiba,” pasipo kuwapatia mahitaji yao ya mwili, kuna faida gani? 17 Vivyo hivyo imani peke yake kama haina matendo, imekufa.
18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nita kuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. 19 Unaamini kuwa kuna Mungu mmoja. Vema. Lakini hata mashetani huamini hivyo, nao hutetemeka!
20 Ewe mpumbavu, unataka ushahidi wa kuthibitisha kwamba imani bila matendo ni bure? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesa biwa haki kwa matendo, alipomtoa mwanae Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake na imani ikakamilishwa kwa matendo. 23 Kwa njia hiyo yaka timizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akahesabiwa kuwa mtu mwenye haki”; naye akaitwa rafiki wa Mungu.
24 Mnaona kwamba mtu huhesabiwa haki kwa matendo wala si kwa imani peke yake. 25 Hali kadhalika Rahabu, yule kahaba, yeye je, hakuhesabiwa haki kwa matendo yake alipowapokea wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo imekufa.
Yesu Ajaribiwa Na Shetani
4 Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini 2 akijaribiwa na shetani. Siku zote hizo hakula cho chote , kwa hiyo baada ya muda huo aliona njaa.
3 Shetani akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika maandiko, ‘mtu haishi kwa chakula tu.’ ”
5 Kisha shetani akamchukua hadi juu ya mlima mrefu akamwo nyesha kwa mara moja milki zote za dunia. 6-7 Akamwambia, “Uki piga magoti na kuniabudu, nitakupa uwezo juu ya milki zote hizi na fahari yake; maana ni zangu na ninaweza kumpa ye yote nita kaye.” 8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.’ ”
9-11 Ndipo shetani akamfikisha Yerusalemu, akampand isha juu ya mnara wa Hekalu, akamwambia: “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kwani imeandikwa, ‘Mungu ataamrisha mal aika wake wakulinde
12 Yesu akamwambia, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
Mungu wako.’ ”
13 Basi Shetani alipomaliza majaribu yote, akamwacha Yesu kwa muda.
Yesu Ahubiri Galilaya
14 Kisha Yesu akarudi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zikaenea katika sehemu zote za wilaya ile. 15 Alifundisha katika masinagogi yao na wote wakamsifu.
Yesu Akataliwa Na Watu Wa Nazareti
16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifun gua mahali palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.” 20 Akakifunga kitabu, akamrud ishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Ndipo akasema: “Maandiko haya mliyosikia nikisoma, leo yametimia.”
22 Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake mazuri, wakaulizana, “Je, huyu si yule mtoto wa Yusufu?” 23 Lakini akawajibu, “Bila shaka mtaniambia, ‘Daktari, jiponye! Mbona hutendi hapa kijijini kwako miujiza tuliyosikia kuwa umeifanya kule Kapernaumu?’ 24 Ningependa mfahamu ya kwamba hakuna nabii anayekubaliwa na watu kijijini kwake. 25 Nawahakik ishieni kwamba walikuwepo wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mvua ilipoacha kunyesha kwa miaka mitatu na nusu, pakawepo na njaa kuu nchi nzima. 26 Lakini Eliya hakutumwa kumwokoa hata mmojawapo wa hawa wajane, isipokuwa alitumwa kwa mjane mmoja wa kijiji cha Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 Na pia wakati wa nabii Elisha, walikuwepo wakoma wengi katika Israeli; lakini hakumtakasa hata mmoja wao, ila Naamani ambaye alikuwa raia wa Siria.”
Siria.”
28 Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, waka kasirika sana. 29 Wakasimama wote wakamtoa nje ya mji hadi kwe nye kilele cha mlima ambapo mji huo ulijengwa ili wamtupe chini kwenye mteremko mkali. 30 Lakini yeye akapita katikati yao akaenda zake. Yesu Afukuza Pepo Mchafu
31 Kisha akaenda Kapernaumu, mji ulioko wilaya ya Galilaya, na siku ya sabato akawafundisha watu katika sinagogi. 32 Walis taajabishwa na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. 33 Alikuwepo mtu mmoja katika sinagogi aliyekuwa ame pagawa na pepo mchafu, naye alianza kupiga kelele kwa nguvu akisema, 34 “Unataka kutufanya nini, Wewe Yesu wa Nazareti? Ume kuja kutuangamiza? Nakufahamu wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Yesu akamwamuru yule pepo: “Nyamaza! Mtoke!” Yule pepo akamwangusha chini yule mtu mbele yao, akamtoka pasipo kumd huru. 36 Watu wote wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho ya mtu huyu ni ya ajabu. Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka! 37 Habari zake zikaenea pote katika mkoa ule.
Yesu Awaponya Wengi
38 Alipotoka katika sinagogi Yesu alikwenda nyumbani kwa Simoni na alipofika huko alimkuta mama mkwe wa Simoni ana homa kali. Wakamwomba sana amponye. 39 Basi Yesu akasimama kando ya kitanda chake akaiamuru ile homa imtoke. Homa ikamtoka yule mama. Akaamka mara moja akaanza kuwahudumia. 40 Jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwa Yesu. Akamgusa kila mgonjwa, akawaponya wote. 41 Pepo wachafu pia waliwatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walifahamu kuwa yeye ni Kristo.
42 Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, na walipom wona wakajaribu kumzuia asiondoke. 43 Lakini yeye akawaambia, “Ninao wajibu wa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu sehemu nyingine pia. Hii ndio sababu nilitumwa.” 44 Kwa hiyo akaende lea kuhubiri katika masinagogi ya Yudea. Yesu Awachagua Wanafunzi Wa Kwanza
Copyright © 1989 by Biblica