M’Cheyne Bible Reading Plan
Tuige Mfano Wa Yesu
12 Basi na sisi kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi inay otusonga kwa urahisi; tupige mbio kwa ustahimilivu katika mashin dano yaliyowekwa mbele yetu. 2 Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Mtafakarini yeye aliyestahimili uadui wa namna hii kutoka kwa wenye dhambi; msije mkachoka wala kufa moyo. 4 Katika kushin dana kwenu na dhambi, bado hamjapigana na majaribu kiasi cha kufikia hatua ya kumwaga damu yenu. 5 Je, mmekwisha sahau yale maneno ya kuwatia moyo, yanayowataja kama wana? “Mwanangu, usid harau nidhamu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya. 6 Maana Bwana huwaadhibu wale awapendao na humpiga kila anayemkubali kuwa ni mwanae.”
7 Vumilieni mateso kama mafunzo. Mungu anawatendea kama wanawe. Maana ni mwana yupi asiyeadhibiwa na baba yake? 8 Kama mtaachiwa bila kuwa na nidhamu, na kila mtu hufundishwa kuwa na nidhamu, basi ninyi ni wana haramu, si wanawe wa halali. 9 Zaidi ya hayo, baba zetu waliotuzaa walituadhibu nasi tukawaheshimu kwa ajili hiyo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa baba wa roho zetu ili tuishi? 10 Baba zetu wa hapa duniani walituadhibu kwa muda mfupi kama wao wenyewe walivyoona kwamba inafaa. Lakini Mungu anatuadhibu kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Adhabu yo yote huonekana kuwa kitu cha kuumiza na kisichofu rahisha wakati ule inapotolewa. Lakini baadaye, matunda yake kwa wale waliofundishwa kwa nidhamu hiyo, ni haki na amani.
12 Kwa hiyo imarisheni mikono yenu iliyolegea na magoti yenu yaliyo dhaifu. 13 Nyosheni njia za miguu yenu ili mguu ulioumia usilemae, bali upone.
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15 Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi. 16 Hakik isheni kwamba miongoni mwenu hamna mwasherati au mtu asiyemcha Mungu. Kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja, aliuza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza. 17 Maana mnafahamu ya kwamba baadaye, alipotaka kurithi ile baraka aliyokuwa apewe, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.
18 Hamkuja kukaribia mlima ambao unaweza kuguswa, na ambao unawaka moto; wala hamkuja kwenye giza, huzuni na dhoruba, 19 na mlio wa tarumbeta na sauti ikisema maneno kwa kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno lingine zaidi. 20 Kwa maana hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Kama hata mnyama atag usa mlima huu, atapigwa mawe.” 21 Kwa hakika waliyoona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” 22 Lakini ninyi mmekuja kwenye Mlima wa Sioni, na kwenye mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, ambapo wamekusanyika kwa shangwe maelfu na maelfu ya malaika. 23 Mmefika kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu ambao majina yao yameandikwa mbin guni. Mmekuja mbele ya Mungu, hakimu wa watu wote, na mbele ya roho za watu wenye haki, waliofanywa wakamilifu. 24 Mmefika kwa Yesu, msuluhishi wa agano jipya, na kwa damu ile iliyonyunyizwa, inenayo maneno mema kuliko damu ya Abeli.
25 Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa hawa kuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi tutaepukaje tukimkataa yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 26 Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”
27 Maneno haya, “Kwa mara moja tena,” yanaonyesha kwamba vile vinavyotetemeshwa vitaondolewa, yaani vyote vilivyoumbwa, kusudi vibaki vile tu visivyoweza kutetemeshwa.
28 Kwa hiyo, tuwe na shukrani kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna itakay ompendeza, kwa unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto unaoteketeza.
Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti
39 , 40 Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti. 41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa. 43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu! 44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.” 46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana, 47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa. 49 Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu. 50 Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao. 51 Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya. 52 Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge. 53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54 Amem saidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake, 55 kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.” 56 Mar iamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.
Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji
57 Ikawa siku za kujifungua kwake Elizabeti zilipotimia, alizaa mtoto wa kiume . 58 Habari zikawafikia majirani na jamaa jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu. Nao wakafurahi pamoja naye. 59 Mtoto alipokuwa na umri wa siku nane, watu wakaja kuhudhuria tohara yake. Wote wakataka wampe yule mtoto jina la Zakaria, yaani jina la baba yake. 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “La si hilo. Jina lake litakuwa Yohana.” 61 Wakamjibu, “Mbona hakuna mtu katika jamaa yako mwenye jina kama hilo?” 62 Basi wakaamua kumwuliza Zakaria kwa ishara kwamba yeye angependa mtoto aitwe nani. 63 Akaomba mahali pa kuandikia, naye akaandika: “Jina lake ni Yohana.” Watu wote wakastaajabu. 64 Papo hapo uwezo wa kusema ukamrudia Zakaria naye akaanza kumsifu Mungu. 65 Watu wote walioshuhudia jambo hili wakastaajabu mno, na habari hii ikaenea sehemu zote za wilaya ile ya Yudea. 66 Na kila aliyezisikia habari hizi aliwaza moyoni: “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Utabiri Wa Zakaria
67 Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akata biri akisema: 68 “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake ili awakomboe. 69 Naye ametusimamishia nguvu ya wokovu katika ukoo wa Daudi mtumishi wake; 70 kama alivy oahidi kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani: 71 kwamba atatuokoa na maadui zetu na kututoa kutoka katika mikono ya wote watuchukiao. 72 Aliahidi ataonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu 73 aliloagana na baba yetu Ibrahimu: 74 kutuokoa kutoka katika mikono ya adui zetu na kutuwezesha kumtumikia pasipo woga, 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. 76 Na wewe mwanangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia Bwana na kumwandalia njia; 77 na kuwafahamisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na 79 kuwaangazia wote waishio katika giza na katika uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” 80 Yule mtoto akakua na kuko maa kiroho; akaishi nyikani hadi alipoanza kuwahubiria Waisraeli hadharani.
Copyright © 1989 by Biblica