M’Cheyne Bible Reading Plan
Paulo Aenda Korintho
18 Baada ya haya, Paulo aliondoka Athene akaenda Korintho. 2 Huko alimpata Myahudi mmoja jina lake Akila, mzaliwa wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu mfalme Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona. 3 Akakaa nao na kufanya kazi na Akila kwa sababu wote wawili walikuwa mafundi wa kutengeneza mahema. 4 Kila siku ya sabato Paulo alikwenda katika sinagogi akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki waamini. 5 Sila na Timotheo walipofika kutoka Makedonia walimkuta akihubiri na kuwashuhudia Wayahudi na Wagiriki, kuwa Yesu ndiye Kristo. 6 Wal ipombishia na kumtukana alikung’uta mavazi yake akawaambia, “Mimi sina lawama, mkipotea , lawama iko juu yenu wenyewe. Tangu sasa nitawahubiria mataifa neno la Mungu.” 7 Kwa hiyo Paulo akaondoka akaenda kwenye nyumba ya mtu anayeitwa Titio Yusto ali yekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa karibu sana na sinagogi. 8 Kiongozi wa hilo sinagogi aliyeitwa Krispo akamwamini Bwana pamoja na jamaa yake; na Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa. 9 Usiku mmoja Bwana akazungumza na Paulo katika ndoto akamwambia, “Usiogope, endelea kuhubiri wala usi kate tamaa. 10 Kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia na kukudhuru; kwa kuwa kuna watu wengi walio wangu katika mji huu.” 11 Kwa hiyo Paulo akakaa Korintho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, akiwafundisha waamini neno la Mungu. 12 Lakini wakati Galio alipofanywa kuwa Liwali wa Akaya, Wayahudi waliungana kumshambulia Paulo, Wakamkamata na kumpeleka Mahakamani. 13 Wakamshitaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria zetu.” 14 Paulo alipo taka kujitetea Galio akawaambia Wayahudi, “Kama mashtaka yenu yalihusu makosa ambayo mtu huyu amefanya au kama yangehusu ujam bazi, ningewasikiliza. 15 Lakini kwa kuwa kesi hii inahusu maneno na majina yaliyo katika sheria zenu, itawabidi muiamue wenyewe. Nakataa kabisa kujihusisha na jambo hili.” 16 Akawafu kuza kutoka mahakamani. 17 Wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya mahakama. Wala Galio hakuingilia kati.
Paulo Arudi Antiokia
18 Baada ya haya Paulo alikaa huko Korintho kwa siku nyingi zaidi kisha akaagana na wale ndugu waamini akasafiri kwa meli kuelekea Siria akiongozana na Prisila na Akila. Walipofika Kenk rea Paulo alinyoa nywele zake kwa maana alikuwa ameweka nadhiri. 19 Walipofika Efeso Paulo aliwaacha Prisila na Akila, akaenda katika sinagogi akawa akijadiliana na Wayahudi. 20 Walipomwambia akae nao kwa muda mrefu zaidi alikataa, 21 lakini alipokuwa aki waaga aliwaambia, “Nitarudi kama Mungu akipenda.” Akasafiri kwa meli kutoka Efeso. 22 Alipofika Kaisaria alikwenda kuwasalimu ndugu katika kanisa kisha akaelekea Antiokia. 23 Alikaa Antiokia kwa muda, na baadaye aliondoka akatembelea makanisa huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha waamini wote.
Apolo Ahubiri Efeso Na Korintho
24 Basi Myahudi mmoja jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksan dria alikuja Efeso. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhu biri na pia aliyajua Maandiko barabara. 25 Alikuwa amefundishwa njia ya Bwana naye akiwa amejaa moto wa kiroho alifundisha kwa usahihi juu ya Yesu. Lakini ujuzi wake uliishia kwenye ubatizo wa Yohana. 26 Apolo alihubiri kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27 Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28 maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.
Yesu Anatabiri Kubomolewa Kwa Hekalu
13 Alipokuwa akitoka nje ya Hekalu, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, ona jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo maridadi!”
2 Yesu akamjibu, “Unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomo lewa.”
Yesu Anawaambia Wafuasi Wake Wajiandae Kwa Mateso
3 Alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni akiliangalia Hekalu, Petro, Yakobo na Yohana walimwuliza faraghani, 4 “Tafadhali tuambie, mambo haya yatatokea lini, na ni ishara gani zitaonyesha kuwa karibu yatatimia?” 5 Yesu akaanza kuwaeleza: “Jihadharini mtu asije akawadanganya. 6 Wengi wata kuja wakilitumia jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye’ na wata wadanganya wengi. 7 Na mkisikia habari za vita na uvumi juu ya vita, msishtuke. Mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho utakuwa bado. 8 Mataifa yatapigana na falme kushambuliana. Matetemeko ya ardhi yatatokea sehemu mbalimbali na kutakuwa na njaa. Lakini huu utakuwa kama maumivu ya mwanzo tu ya uchungu wa uzazi. 9 Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watu watawapeleka mahakamani na mtapigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ndipo mtaweza kutoa ushuhuda kuhusu Habari Njema. 10 Lakini kabla mwisho kufika, Habari Njema itahubiriwa kwa mataifa yote. 11 “Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.
12 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 13 Kila mtu atawachukia kwa ajili yangu; lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
14 “Mtakapoona ile ‘sanamu ya chukizo’ imesimama mahali isipostahili - msomaji na aelewe maana yake -basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 15 Mtu aliyeko juu ya nyumba asiter emke kuingia ndani kuchukua cho chote. 16 Aliyeko shambani asi rudi nyumbani kuchukua koti lake. 17 Ole wao akina mama waja wazito na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 18 Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa masika. 19 Kwa maana siku hizo itaku wapo dhiki kuu ambayo haijapata kutokea tangu dunia ilipoumbwa, wala haitatokea tena. 20 Na kama Bwana hakuufupisha muda huo wa dhiki, hakuna mtu ambaye angesalimika; lakini kwa ajili ya watu wake aliowachagua, ameufupisha muda huo.
21 “Na wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa’ au , ‘Tazama, yule pale,’ msiamini. 22 Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watafanya ishara na miujiza ili kuwadanganya hata wale waliochaguliwa na Mungu, kama ikiwezekana. 23 Kwa hiyo jihadharini kwa maana nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
24 “Siku hizo, baada ya hiyo dhiki, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake. 25 Nyota zitaanguka kutoka mbinguni na nguvu za anga zitatikisika. 26 Ndipo watu wote wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utu kufu. 27 Nami nitawatuma malaika wawakusanye watu wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa nchi hadi mwisho wa mbi ngu.
28 “Sasa jifunzeni jambo hili kutoka kwa mtini: mwonapo matawi ya mtini yakianza kulainika na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29 Hali kadhalika mtaka poyaona mambo haya yanatokea, tambueni kwamba mimi Mwana wa Adamu, ni karibu kuja. 30 Ninawaambieni hakika, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo haya kutokea. 31 Mbingu na nchi zita toweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa
32 “Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake. 33 “Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi. Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36 Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37 Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”
Copyright © 1989 by Biblica